Tuesday, July 12, 2016
GWAJIMA ARUDI NA KQ ASHIKWA
Do you like this story?
Hatimaye
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye amekuwa akitafutwa
na Jeshi la polisi kwa siku kadhaa alikamatwa jana katika uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere (JNIA) alipowasili alitokea japan.
Baada
ya Askofu Gwajima kukamatwa na kikosi cha Polisi Uwanja wa JNIA alipelekwa moja
kwa moja kituo cha polisi kwa ajili ya
mahojiani akidaiwa alitoa maneno ya uchochezi mwezi uliopita.
Akizungumzia
kukamatwa kwake, kamanda wa polisi
Askofu huyo aliwasili saa 2.45 asubuhi akitokea Japan kwa kutumia ndege
ya shirika la ndege la Kenya.
Otieno
alisema mara baada ya kukamatwa alipelekwa katika kituo kikuu cha polisi kwa
ajili ya kuhojiwa na jeshi la polisi kanda maalum ya dar es salaam.
“Ni
kweli tulikamata Askofu Gwajima hapa uwanja wa ndege wa JNIA baada ya kuwasili
kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya na tulipomuhoji alidai kuwa alikuwa
nchini Japan” alisema Otieno.
Mwanasheria
wake Peter Kabatala alisema Gwajima alifika kituo cha polisi saa 4:45 asubuhi
kwa mahojiano mafupi na aliruhusiwa kuondoka baada ya kujiadhamini yeye
mwenyewe.
“Askofu
Gwajima amehojiwa leo (jana) na jeshi la polisi kanda maalumu na amejidhamini yeye mwenyewe,
ameruhusiwa kuondoka hivyo tunasubiri chochote kitakachoendelea” alisema
Kibatala bila kueleza mahojiano yalivyokuwa.
Askofu
Gwajima alikuwa anatafutwa na polisi tangu mwezi uliopita baada ya kusambazwa
mkanda kwenye mitandao ya kijamii unaodhaniwa una sauti yake akipendekeza Rais
mstaafu Jakaya Kikwete kufikishwa mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa
utawala wake ambayo sasa Rais John Magufuli anayashughulikia kwa mtindo wa
kutumbua majipu.
Katika
mkanda huo, sauti hiyo inadai kuwa
baadhi ya viongozi wa CCM wametuma watu mikoani kupiga kampeni ya kutaka Rais
Magufuli asipwe uongozi wa chama hivo kwa sasa kama ilivyo utaratibu wa chama
hicho na kwamba hili likifanyika basi Rais abadili katiba ili mstafu huyo aweze
kufikishwa kortini.
Tangu
ulipotolewa mkanda huo makachero wa polisi wamekuwa wakipiga kambi nyumbani kwa
Askofu Gwajima kwa lengo la kumkamata lakini hawakumpata. Baadaye ilikuja
kufahamika kwamba Askofu huyo alikuwa amekwenda nje ya nchi lakini
haikujulikana ni nchi gani.
Hata
hivyo baada ya kutafutwa na polisi Gwajima kupitia wakili wake Kibatala alisema
atakaporejea nchini atakwenda moja kwa moja polisi kwa ajili ya mahojiano.
Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amekuwa akisisitiza
kwamba jeshi litaendelea kumtafuta askofu huyo kwa kushirikiana na polisi wa kimataifa, Interpol.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “GWAJIMA ARUDI NA KQ ASHIKWA ”
Post a Comment