Tuesday, July 5, 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA ATEMBELEA PANDAHILL PATAKAPOCHIMBWA MADINI ADIMU DUNIANI.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala akitoa pongezi kwa Kampuni ya Panda hill iliyowekeza katika Mkoa wa Mbeya katika kuchimba Madini ya aina ya
Niobium.


Mwonekano wa Bonde la Songwe.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Meneja Mr Derek Oliver akiongea na Waandishi wa Habari.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (kushoto)akionyeshwa Ramani na Meneja Mr Derek Oliver Jinsi watakavyo chimba madini hayo yajulikanayo kama Niobium.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Emmanuel Kisasi akitoa ufafanuzi kuhusu Madini hayo Ambayo itakuwa ndio ya kwanza Afrika.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (kushoto)akionyeshwa Ramani na Meneja Mr Derek Oliver Jinsi watakavyo chimba madini hayo yajulikanayo kama Niobium.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Mwonekano wa Ramani jinsi watakavyofanya kazi katika maeneo hayo ya songwe.



Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo ametembelea eneo la Pandahill kata ya Songwe mahali ambapo patachimbwa madini adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer na mpaka sasa madini hayo huchimbwa bara la Amerika tu na kugundulika kwa madini hayo Tanzania utakuwa mgodi wa nne duniani na wa kwanza Afrika.

Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick amesema imewachukua zaidi ya miaka 5 kufanya utafiti na kugundua uwepo wa madini hayo, taratibu zote za kisheria zimekamilika na kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika mradi huo na mradi utatengeneza ajira watu 500 na mradi huo utaanza uzalishaji mapema mwaka 2018.

Mkuu wa mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ugunduzi na uwekezaji huo mkubwa na akawataka washirikiane na viongozi na wananchi kwa kila hatua ili kuweka wazi mradi huo kwa wananchi

Aidha amewataka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ili wananchi wanaozunguka eneo hilo uzalishaji utakapoanza wafaidike na ajira, huduma za jamii na kodi mbalimbali kwa halmashauri na serikali kuu.

0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA ATEMBELEA PANDAHILL PATAKAPOCHIMBWA MADINI ADIMU DUNIANI.”

Post a Comment

More to Read