Tuesday, July 12, 2016

NATAKA JIJI LA MBEYA LIWE LA MFANO KWA USAFI HAPA NCHINI-RC MBEYA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala akizindua rasmi magari ya kubeba Uchafu yaliyotolewa kwa msaada wa Benk ya Dunia.(picha na David Nyembe wa Fahari News)

Moja ya Gari ambalo limekodiwa na jiji la Mbeya kwaajili ya kubeba uchafu maeneo ya Uhindini jijini Mbeya.(picha na David Nyembe wa Fahari News)


Mwonekano wa Makontena Hayo.(picha na David Nyembe wa Fahari News)

Baadhi ya wakina mama wakiwa wanafanya Biashara zao Mbele ya uchafu.(picha na David Nyembe wa Fahari News)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (mwenye miwani)akiwa na katibu Tawala(kulia) naibu Meya pamoja na Kaimu Mkurugenzi.wakiwa wametoka kukagua makontena hayo.(picha na David Nyembe wa Fahari News)




SERIKALI Mkoani Mbeya imesema licha ya jitihada zilizoonekana kuchukuliwa na halmashauri ya Jiji la Mbeya katika suala la usafi bado jiji hilo ni chafu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala, amesema bado jitihada za dhati zinahitajika kuchukuliwa na maafisa wa Jiji hilo ili kuhakikisha Jiji linakuwa safi kwa kulinda hadhi yake.


Mkuu  wa Mkoa aliyasema hayo baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya kutolea taka yakiwemo magari matano na kontena 91 za kuhifadhia taka zilizotolewa kupitia mradi wa benki ya dunia.

Amesema, licha ya kuwepo kwa sheria ndogo za usimamizi wa usafi wa mazingira   lakini jiji la Mbeya bado ni chafu na kuwataka watendaji kupanga mikakati itakayohakikisha Jiji la Mbeya inashika nafasi ya kwanza kwa usafi kwenye ngazi za majiji nchini.


Katika kuhakikisha suala hilo linatekelezeka Makala, alilazimika kutoa siku kadhaa kwa uongozi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha unasimamia na kutekeleza sheria za usafi wa mazingira kwa vitendo.

Amesema, watendaji wamekuwa wakitoa visingizio visivyokuwa na sababu zozote za msingi  zinazohusiana na suala zima la usafi, ninachowashauri ni kufanya kazi kama sheria za kazi zinavyoelekeza.

“Kuanzia leo naomba mnisikie  kwa makini endapo mtendaji anaona ameshindwa kazi ni vema akaacha  kwani  serikali haiwezi kuwalipa mishahara watu ambao hawatambui wajibu wao kwa jamii ni upi,”alisema

Aidha, Makala aliutaka uongozi huo kutambua kuwa  wafanyabiasha wadogowadogo ni sehemu ya jamii hivyo wajibu wao ni kuwapanga vizuri kwa kuwatafutia maeneo na si kugombana nao.

Akizungumzia hilo, Kaimu Naibu Meya wa Jiji la Mbeya, Gofrey Kajigili ambaye ni Diwani wa Kata ya Sisimba, alisema suala la kukithiri kwa hali ya uchafu ndani ya Jiji la Mbeya linachangiwa na uelewa mdogo wa watendaji wa serikali  ngazi za mitaa.



0 Responses to “NATAKA JIJI LA MBEYA LIWE LA MFANO KWA USAFI HAPA NCHINI-RC MBEYA ”

Post a Comment

More to Read