Wednesday, July 13, 2016

NJOMBE KIDEDEA KAMPENI YA USAFI, YATWAA TOYOTA LAND CRUISER.


Waziri Mwalimu (kushoto) akiwa na baadhi ya wawakilishi wa Halmashauri ya Mkoa wa Njombe.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  akiwakabidhi cheti baadhi ya wawakilishi kutoka halmashauri zao.

Baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa halmashauri zilizoibuka kidedea kwa usafi.

Gari la ushindi wa Halimashauri ya Njombe.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Njombe, Valentino Aidani,  akiwa ndani ya gari walilojishindia.


HALMASHAURI ya Mkoa wa Njombe leo imeimbuka kidedea na kutwaa gari aina ya  ‘Toyota Land Cruiser’ na pikipiki  baada ya kutangazwa mshindi katika Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira ulioanza mwaka jana.

Halmashauri hiyo imeibuka kidedea leo katika hafla fupi iliyofanyika Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya ambao walikabidhi zawadi za medali na vyeti vya ushindi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwalimu amesema kuwa tangu kampeni hiyo ya kufanya usafi kuzinduliwa na Rais John Pombe Magufuli,  wananchi kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuwa mabalozi wazuri katika kuhakikisha mazingira wanayoishi yapo safi na kuhimizana kuendelea na usafi wa mazingira kuepukana na ugonjwa wa kipindupindu na kuishi kwenye mazingira ya kuvutia.

Aidha aliziasa halmshauri zote nchini kuhakikisha zinaiga mfano kutoka Halmashauri ya Njombe iliyoibuka kidedea ili ziweze kuwa miongoni mwa washindi wa zawadi nyingine.

Halmashauri ya Njombe iliibuka kidedea katika nyanja mbalimbali za vigezo vilivyokuwa vikizingatiwa ikiwemo mitaa zao za mkoa huo.

Kwa upande wa halmashauri za miji zilizoibuka kidedea ni Halmashauri ya Mbeya na ya Kinondoni huku kwa upande wa manispaa ni Iringa, Moshi na Mpanda.

0 Responses to “NJOMBE KIDEDEA KAMPENI YA USAFI, YATWAA TOYOTA LAND CRUISER.”

Post a Comment

More to Read