Wednesday, July 13, 2016
WATUMISHI HEWA WAISABABISHA SERIKALI KUSITISHA AJIRA MPYA ZA WATUMISHI 71,496
Do you like this story?
WAZIRI wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella
Kairuki amesema serikali imelazimika kusitisha ajira mpya za watumishi 71,496
serikalini, mwaka huu hadi pale tatizo la watumishi hewa litakapopatiwa
ufumbuzi.
Akifungua
mafunzo kuhusu maadili ya viongozi wa umma kwa wakurugenzi watendaji wa
halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji Ikulu Dar es Salaam jana,
Kairuki alisema tangu oparesheni ya kutafuta watumishi hewa ianze hadi sasa
watumishi 12,246 wameshaondolewa.
Kairuki
alisema tatizo la watumishi hewa nchini bado ni kubwa kwani uzoefu unaonesha
kuwa nchi nyingi zilizokumbwa na tatizo hilo, ni asilimia ndogo tu ya watendaji
ndio iliyokuwa inawajibika.
Alisema
kwa sasa serikali imelazimika kusimamisha masuala mengi ya utumishi wa umma ili
ipate taarifa kamili ya aina ya watumishi waliopo, na kwamba ma-DED hao kuhakikisha
wanasimamia vyema oparesheni hiyo kwani hadi sasa watumishi hewa waliobainika,
takribani asilimia 90 wanatokea katika Serikali za Mitaa.
Aidha,
Kairuki alisema pamoja na kugundulika kuwa tatizo la watumishi hewa ni kubwa
nchini, pia serikali imebaini kuwepo kwa watumishi watoro wasiotimiza wajibu
wao.
“Nawataka
mkahakikishe mnawabana hawa maofisa utumishi, haiwezekani kuwepo na tatizo la
watumishi hewa kubwa kiasi hiki huku pia kukiwa na tatizo la watumishi watoro,
hawa maofisa kwani walikuwa na majukumu gani?” Alihoji Kairuki.
Alisema
endapo serikali itabaini kuwa maofisa utumishi hao wamehusika katika matatizo
hayo ya watumishi hewa na utoro, wataondolewa mara moja.
“Serikali haina mchezo kila ofisa katika eneo lake, awe ofisa elimu, afya na kilimo wafanye kazi zao,” alisema.
“Serikali haina mchezo kila ofisa katika eneo lake, awe ofisa elimu, afya na kilimo wafanye kazi zao,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATUMISHI HEWA WAISABABISHA SERIKALI KUSITISHA AJIRA MPYA ZA WATUMISHI 71,496”
Post a Comment