Wednesday, July 13, 2016
MKUU WA MKOA WA MBEYA AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA SHEREHE NA MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE 2016,WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI KILELE AGOSTI 8-
Do you like this story?
Wakuu wa Wilaya. |
wanahabari. |
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amezitaka halmashauri za mikoa 7 ya nyanda za juu
kusini , washiriki, wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha maonyesho ya
nanenane mwaka huu yatakuwa ya mfano hivyo amewataka kujipanga na kufanya
maandalizi mazurii kuliko maonyesho ya kanda zingine
Hayo yamesemwa leo jijini Mbeya katika kikao cha maandalizi ya maonyesho ya nanenane ya nyanda za juu kusini yanayojumuisha mikoa 7 ambayo ni Mbeya,iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma,Rukwa na Katavi.
Aidha amekieleza kikao hicho kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonyesho hayo tarehe 1 /8/2016 atakuwa Dr Charles Tizeba( Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi) na kilele cha maonyesho hayo itakuwa tarehe 8/8/2016 na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano Kassim Majaliwa( mb)
Hivyo amewaaomba washiriki, wadau na wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA SHEREHE NA MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE 2016,WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI KILELE AGOSTI 8-”
Post a Comment