Wednesday, August 10, 2016
MABADILIKO YA RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA.
Do you like this story?
Kutokana na sababu mbalimbali,
Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imelazimika
kubadili Ratiba ya Ligi Kuu kwa michezo kadhaa ya mwanzo kama ifuatavyo.
1. Mchezo Na. 2 – Kagera Sugar vs
Mbeya City (20.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe
21.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Sababu ni kuwa uwanja wa
Kaitaba bado utakuwa kwenye matengenezo.
2. Mchezo Na.4 – Toto African vs
Mwadui FC (20.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe
24.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kirumba. Sababu za mabadiliko ni kuwa uwanja
huo tarehe 20.08.2016 utakuwa na matumizi mengine ya kijamii.
3. Mchezo Na.13 – Kagera Sugar vs
Stand United (27.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa katika
Uwanja wa CCM Kambarage. Awali timu mwenyeji wa mchezo huo ilikuwa ni Kagera
Sugar, lakini kwa sasa timu mwenyeji atakuwa ni Stand United.
4. Mchezo Na.55 – Toto vs Ndanda
(02.10.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe
03.10.2016 badala ya tarehe 02.10.2016
5. Mchezo Na.80 – Mbao FC vs
Ndanda fc (16.10.2016)
Mchezo huo umerudishwa nyuma
kutoka tarehe 16.10.2016 hadi tarehe 28.09.2016. Sababu ni kuiwezesha timu ya
Ndanda kucheza michezo miwili kwa kanda ya ziwa kwa lengo la kupunguza gharama.
6. Mchezo Na.96 – Tanzania
Prisons vs Mbao FC (22.10.2016)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MABADILIKO YA RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA.”
Post a Comment