Wednesday, August 10, 2016
WAZIRI MBARAWA ZINDUA TRENI YA PILI DAR.
Do you like this story?
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amezindua treni ya pili
ya abiria jijini Dar es Salaam, inayofanya safari zake kuanzia kituo kikuu cha
stesheni hadi Pugu.
Akizungumza mara baada ya kuzindua treni hiyo Waziri Mbarawa amesema kuwa serikali imejipanga usafiri huo kuwa endelevu ili kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Waziri
Mbarawa amesema treni hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 1500 kwa wakati mmoja
itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa msongamano na kuwahisha shughuli za
maendeleo kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Aidha
waziri Mbarawa amesema kuwa takribani magari 46 yanayobeba abiria 35 yatakuwa
yamepungua kutokana na treni hiyo ambayo licha ya changamoto zilizokuwepo
ameahidi kushughulikia ili usafari huo uweze kudumu kwa muda mrefu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAZIRI MBARAWA ZINDUA TRENI YA PILI DAR.”
Post a Comment