Tuesday, August 9, 2016
WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA AGUNDUA UFISADI WA KUTISHA SOKO LA MWANJELWA....AMUAGIZA CAG AFANYE UKAGUZI
Do you like this story?
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akipata Maelezo kuhusu Biashara zinavyoendelea katika soko la Mwanjelwa(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akisalimiana na Meya wa Jiji la Mbeya Mch David Mwashilindi mara baada ya kuwasili. |
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la la Mbeya Mussa Mapunda mara baada ya kuwasili katika soko la Mwanjelwa |
Waziri Mkuu akizungukia Soko kuona Maendeleo yake leo |
Wananchi walijitokeza kwa wingi kumsikiliza Waziri Mkuu kwenye Soko Jipya la Mwanjelwa Jijini Mbeya |
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya baada
ya kuwepo kwa ubadhilifu katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa.
“Inasikitisha
ujenzi wa soko hili kuingia ubabaishaji. Ujenzi wa soko ungegharimu sh bilioni
16 ila sasa watendaji wamefanya mambo ya hovyo na kufikia sh bilioni 26
hatuwezi kuwavumilia lazima hatua zichukuliwe kwa wote watakaobainika katika
ubadhilifu huu,” alisema.
Pia amempa
siku tatu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kufanya uchunguzi na kubaini nani
aliyetafuna sh milioni 489 zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya
uendelezaji wa soko hilo ambazo hazijulikani zilipo.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 09, 2016) wakati alipofanya ziara
ya kushitukiza katika soko la Mwanjelwa na kubaini ubadhilifu wa fedha katika
ujenzi wa soko hilo.
Waziri
Mkuu amesema mara baada ya CAG kumaliza kufanya ukaguzi atatoa taarifa na mtu
yeyote atakayetajwa katika ripoti hiyo kuwa amehusika na ubadhilifu huo
atawajibika hata kama yuko nje ya Jiji la Mbeya.
Alisema
kitendo cha kuongeza gharama za ujenzi wa soko hilo kutokana na kuchelewa kwa
ujenzi wake kinaisababishia Halmashauri yaJiji kulipa sh milioni 200 kila mwezi
kwa ajili ya marejesho, hivyo aliagiza aliyesababisha gharama hizo asakwe na
achukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Wakati huo
huo Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa Mkoa Mbeya, Amos Makalla kuhakikisha mtu
aliyepangishwa katika kibanda cha kukusanyia uchafu sokoni hapo anaondolewa
haraka na kurudishiwa fedha zake ili kibanda hicho kitumike kama
ilivyokusudiwa.
Pia
alimuagiza Mkuu huyo wa Mkoa kufanya ukaguzi katika vyumba vya maduka sokoni
hapo na ifikapo Jumatatu mtu hajaweka mali anyang’anywe na kupangishwa kwa mtu
mwingine mwenye kuhitaji.
Alisema
hayo baada ya baadhi ya wafanyabiashara kulalamika kuwa kuna watu wamechukua
vyumba vingi vya maduka kwa ajili ya kuvipangisha kwa wafanyabiashara kwa
gharama kubwa tofauti na inayotozwa na Halmashauri, hivyo kunyima nafasi kwa
walengwa kunufaika na soko hilo.
Mmoja wa
wajasiriliamali sokoni hapo Mohammed Said alisema watu wameshika vyumba na
kuviuza kwa sh milioni 20 hadi 40 kulingana na eneo kilipo chumba jambo
linalosababisha baadhi ya wafanyabiashara kushindwa kupata nafasi katika soko
hilo.
Awali Mkuu
wa Mkoa alisema soko hilo linakabiliwa na matatizo mbalimbali kwani hata
wahanga waliokuwa wanafanya biashara kabla ya soko kuungua moto hawakupewa
kipaumbele wakati wa upangishaji wa vyumba vya maduka.
Kuhusu
suala la kukosekana kwa wateja sokoni hapo Makalla amewataka wafanyabiashara
wote wanaofanya shughuli zao katika maeneo yasiyokuwa rasmi kuhamia sokoni hapo
mara moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA AGUNDUA UFISADI WA KUTISHA SOKO LA MWANJELWA....AMUAGIZA CAG AFANYE UKAGUZI”
Post a Comment