Tuesday, August 9, 2016
VYUO VYA UDEREVA VISIVYO NA SIFA MBIONI KUFUNGIWA
Do you like this story?
JESHI la
Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litavifungia vyuo vyote
vinavyotoa mafunzo ya udereva nchini bila ya kuwa na sifa.
Kauli hiyo
ameitoa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP)
Mohamed Mpinga wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za
Udereva Tanzania (Chashubuta) uliofanyika Dar es Salaam jana.
"Kuanzia
sasa Jeshi la Polisi halitasita kukifungia chuo chochote cha udereva
kitakachokosa sifa kwani kwa kulea shule mbovu tutaendelea kupata ajali na
hivyo kuongeza vifo na majeruhi" alisema
Mpinga.
Mpinga
alisema kwa mujibu wa sheria ya shule za udereva sura 163 ya 1965 (R.E 2002)
mpaka sasa jeshi la polisi limesajili shule za udereva 260 ambazo zitategemewa
kutoa madereva bora wenye ueledi wa kutosha kutokana na kuwa chanzo kikubwa cha
ajali ni makosa ya kibinadamu ambayo yanafanywa na madereva.
Alisema
jeshi hilo litafanya msako nchi nzima kuvibaini vyuo ambavyo havina sifa na
wamiliki wake kuchukuliwa hatua na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.
Mwenyekiti
wa Chashubuta Taifa, Robert Mkolla wakati akisoma risala yao mbele ya Mpinga
ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema moja ya changamoto
waliyonayo ni baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri na usafirishaji kutoona
mchango mkubwa unaofanywa na shule za udereva za watu binafsi wakiamini kuwa
vyuo vinavyotoa elimu nzuri ni vile vya serikali pekee.
Mkolla
alimuomba Kamanda Mpinga uboreshwaji wa mitaala mara kwa mara ili kwenda na
mahitaji ya barabara, vyombo na wakati na shule hizo ziwe zinashirikishwa
katika kutoa michango ya uboreshaji wa mitaala hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ VYUO VYA UDEREVA VISIVYO NA SIFA MBIONI KUFUNGIWA”
Post a Comment