Monday, August 1, 2016

MCHUNGAJI AFARIKI AKIOMBA KUPATA MKE





Mchungaji wa Kanisa la maombezi la Mkuburi lililopo Kibangu Jijini Dar es salaam Frank Malusi amekutwa amefariki nyumbani kwake mtaa wa Makaburi Kibangu baada  ya majirani kusikia harufu kali kutoka chumbani kwake
Mchungaji huyo anadaiwa kutoonekana kwa muda wa siku 4 mfululizo ambapo majirani walishtushwa na harufu kali iliyokuwa ikitoka chumbani kwa mchungaji huyo

Kwa mujibu wa majirani wa karibu wa marehemu walisema kuwa  Malusi alikuwa akiishi peke yake na kwa kipindi cha wiki 3 mfululizo zilizopita  alisikika akifanya maombi maalumu  ya kuomba kupata mke

Mwenyekiti wa mtaa huo, Mosha Kaftani amesema kuwa alipewa taarifa na mwenye nyumba ambayo Malusi alikuwa amepanga baada ya mwenye nyumba kupatwa na hofu juu ya harufu kali iliyokuwa ikitoka chumbani kwake na kuwa hakumuona mchungaji huyo akitoka ndani kwake kwa muda wa siku 4

Kaftani alitoa taarifa katika kituo cha Polisi ambapo walikuja na kuvunja mlango na kukuta mwili wa mchungaji huo ukiwa umeanza kuharibika, chanzo cha kifo chake bado hakija julikana na Polisi wapo katika uchunguzi.

0 Responses to “MCHUNGAJI AFARIKI AKIOMBA KUPATA MKE ”

Post a Comment

More to Read