Tuesday, August 2, 2016
WAZIRI AAGIZA NYAMA CHOMA BAA IPIMWE KWA MIZANI.
Do you like this story?
Waziri wa Kilimo na Uvuvi Mh Dk. Charles Tizeba. akizungumza na wananchi katika Maonesho ya Nanenane Mkoa wa Mbeya.(David Nyembe wa Picha na Fahari News) |
Waziri wa Kilimo na Uvuvi Mh Dk. Charles Tizeba akipewa maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa Banki ya NMB kuhusu ukopeshwaji wa Vifaa vya Kilimo. |
Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba ameagiza Wakala wa Vipimo nchini,
kuhakikisha mfumo wa matumizi ya vipimo vya mizani unazifikia huduma za kijamii
zote ikiwemo nyama choma.
Dkt. Tizeba ametoa agizo hilo Agosti Mosi alipokuwa akifungua Maonesho ya Wakulima ya Nanenane, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya na kuhudhuriwa na wadau kutoka halmashauri za mikoa saba ya kanda hiyo.
Amesema miongoni mwa wateja wasionufaika na kile wanachonunua kutokana na kutojua ni kwa kiasi gani wamehudumiwa ni walaji wa nyama hususan zinazochomwa kwa kuwa wauzaji hutumia njia ya kukadiria badala ya kuwapimia.
Amesema jambo la kushangaza ni kuwa wauzaji hao wa nyama choma huchukua bidhaa hizo kwenye bucha na machinjio zikiwa zimepimwa lakini wao hawataki kuwatendea haki wateja wao kwa kuwapimia kwa kipimo kinachotakiwa.
Amesema serikali haiko tayari kuona vipimo vya makopo na ndoo vikiendelea kutumika bali kila mtanzania anapaswa awajibike kwa kuhakikisha kwenye eneo lake matumizi ya vipimo sahihi yanazingatiwa ili kuleta usawa katika uchumi.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAZIRI AAGIZA NYAMA CHOMA BAA IPIMWE KWA MIZANI.”
Post a Comment