Monday, August 8, 2016
MWIGULU NCHEMBA ATANGAZA VITA KWA WAUZA MADAWA YA KULEVYA NCHINI
Do you like this story?
WAZIRI wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa maofisa wanaohusika
na udhibiti wa dawa za kulevya kwenye mpaka wa Tunduma mkoa wa Songwe,
kuwakamata watu wanaohusika na uvushaji wa dawa hizo kutoka nchini kwenda nchi
jirani ya Zambia na nyingine zilizopo ukanda huo.
Nchemba
alitoa agizo hilo jana, alipofanya ziara ya kukagua mpaka huo, ambapo alisema
ni jambo lisilofichika kuwa kwa sasa Tanzania imechafuka kutokana na dawa za
kulevya.
Alisema
kutokana na Watanzania wengi kukamatwa katika nchi mbalimbali duniani,
wakijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya, imefikia hatua kwa baadhi ya
nchi kufikiria kuongeza masharti zaidi kwa kila atakayejitambulisha kuwa
Mtanzania.
“Hatuwezi
kuacha nchi ikachafuka kwa sababu tu ya watu wachache.Ukienda China Watanzania
zaidi ya 200 wanashikiliwa kwa dawa za kulevya, Pakistan wapo, India, Afrika
Kusini ni Watanzania. Hili linatuchafua sana,” alisema Nchemba.
Aliutaja
mpaka wa Tunduma kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kupitisha dawa hizo
na kutaka nguvu kuongezwa zaidi ili kuwezesha misako.
Alisema
wapo watu ambao si makondakta wa mabasi wala abiria, lakini wamekuwa wakisafiri
kila siku kwenye mabasi, hatua inayodhihirisha kuwa ndiyo wanaojihusisha na
usafirishaji wa bidhaa hizo haramu.
Alisema
watu hao wamekuwa na ushirikiano na watu wengine katika miji ya jirani, kabla
ya kufika mpakani ikiwemo kijiji cha Mpemba wilayani Momba mkoani Songwe,
ambapo wakifika hapo basi husimamishwa na mzigo kushushwa, kisha kusafirishwa
kwa njia za panya hadi ng’ambo ya nchi.
“Wakati
ninyi mnafanya utaratibu wa kawaida wa kupitisha gari husika hapa mpakani, wao
wanavusha kupitia njia za panya. Basi likishavuka na mzigo unakuwa umefika
Zambia wanakutana na kuupakia tena kisha wanaendelea na safari.
“Na katika hili ni lazima mzungumze pia na wenzenu wa upande wa pili, wadhibiti pia mji unaofuata baada ya huo wa mpakani maana huko ndiko wanakopakia tena. Kama mtashindwa katika wiki mbili, nitakuja mimi mwenyewe na nitawakamata tu,” alisisitiza.
“Na katika hili ni lazima mzungumze pia na wenzenu wa upande wa pili, wadhibiti pia mji unaofuata baada ya huo wa mpakani maana huko ndiko wanakopakia tena. Kama mtashindwa katika wiki mbili, nitakuja mimi mwenyewe na nitawakamata tu,” alisisitiza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWIGULU NCHEMBA ATANGAZA VITA KWA WAUZA MADAWA YA KULEVYA NCHINI”
Post a Comment