Saturday, August 27, 2016

SIMBA WADINDIWA NA JKT RUVU TAIFA




Mashabiki wa Simba wakishuhudia Mtanange huo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Saalam(Picha na Halid Mhina wa Fahari News Dar es Salaam)




Katika muendelezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania leo wekundu wa Msimbazi Simba walikaribishwa na  Jkt Ruvu katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. 

Mchezo ambao ulikuwa wa kwanza kwa Jkt Ruvu na wa pili kwa Simba ulimalizika kwa kutoka sare ya bila kufungana (0-0)  pale mwamuzi Selemani Kinugani alipo puliza kipenga cha kuashiria mchezo kumalizika.

Licha ya Simba kulishambulia sana goli la Jkt Ruvu katika  kipindi cha pili lakini mikiki yao haikuvuna kitu kwa mlinda mlango wa Jkt Ruvu Said Kipao.



Simba wamegawana point moja moja  na Jkt Ruvu na kufanya kufikisha jumla ya Point 4 wakiwa wameshuka dimbani mara Mbili.

0 Responses to “SIMBA WADINDIWA NA JKT RUVU TAIFA”

Post a Comment

More to Read