Friday, August 26, 2016
JWTZ KUSHEREKEA MIAKA 52 KWA KUTOA HUDUMA BURE KWA WANANCHI
Do you like this story?
Jeshi la
Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kesho linaanza shamrashamra za maandalizi
kuelekea siku ya maadhimisho ya 52 ya majeshi inayotarajiwa kufanyika Septemba
Mosi mwaka huu kwa kufanya usafi na upandaji miti katika kambi za jeshi na
baadhi ya taasisi nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa JWTZ Kanali Ngemela
Lubinga amewatoa hofu wananchi kuwa wasitishike pindi watakapoona wanajeshi
katika maeneo ya karibu na makazi yao.
“Kesho tuaanza
kufanya usafi kuanzia maeneo ya Kawe hadi karibu na kambi ya Lugalo, na kwamba
niwatoe hofu wananchi pindi watakapoona wanajeshi wengi mitaani kwa kuwa hatuna
nia mbaya hivyo wasitufikilie vibaya,” amesema.
Amesema
jeshi hilo litafanya usafi pamoja na upandaji miti katika baadhi ya maeneo
nchini hadi siku ya kilele cha maadhimisho hayo. Pia wanajeshi watajitolea damu
salama katika hospitali za kambi za jeshi.
“Siku kuu
ya majeshi itaadhimishwa pamoja na wanajeshi kujitolea damu kwenye vituo
maalumu vya kutolea damu salama mikoani, katika hospitali zetu za kanda,”
amesema na kuongeza.
“Sanjari
na utoaji damu, madaktari wetu JWTZ watatoa huduma za tiba bure kama upimaji wa
virusi vya Ukimwi, kisukari, na upimaji wa shinikizo la damu. “
“Kama
ilivyo mila na desturi ya majeshi kufanya usafi na utunzaji wa mazingira,
kuelekea siku ya maadhimisho tutafanya usafi na kupanda miti maeneo ya jirani
na kambi na kwenye taasisi za kiraia kadri mahusiano yatakavyofanyika na
taasisi hizo, ” amesema.
Pia
amesema siku hiyo ya maadhimisho itaadhimishwa kwa kuienzi michezo na kudumisha
urafiki baina ya JWTZ, wananchi, na Taasisi na kwamba mashindano mbalimbali
yatafanyika.
Na Regina
Mkonde
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ JWTZ KUSHEREKEA MIAKA 52 KWA KUTOA HUDUMA BURE KWA WANANCHI”
Post a Comment