Thursday, August 11, 2016

ZAMBIA WAPIGA KURA YA URAIS NA WABUNGE LEO





Leo Zambia inaingia kwenye historia ya kufanya  Uchaguzi Mkuu wa kumchagua Rais wa Nchi  pamoja na wabunge watakaoenda kuiongoza Serikali hiyo kwa awamu nyingine.

Ukuaji wa demokrasia unaonekana kukua kwa kasi barani Afrika, baada ya kuwepo kwa upinzani  mkali katika baadhi ya chaguzi barani hapa, hali hii imeonekana tena Nchini Zambia baada ya kuwepo kwa upinzani mkubwa katika kipindi cha kampeni huku vyama viwili vya Siasa kati ya PF chini ya mgombea wake Edgal Lungu ambae ndie Rais kwa sasa na wapinzani wao UPND chini ya mgombea wake Hakainde Hichilema.

Katika kipindi cha kampeni kuriripotiwa kutokea kwa vurugu za kisiasa katika baadhi ya maeneo Nchini Zambia, leo Wananchi hao wanatimiza haiki yao ya kupiga kura kwa ajili ya kumchagua Rais pamoja na wawakilishi wao (wabunge).

0 Responses to “ZAMBIA WAPIGA KURA YA URAIS NA WABUNGE LEO”

Post a Comment

More to Read