Wednesday, September 21, 2016

TCRA YAWANOA WAANDISHI WA HABARI WA NYANDA ZA JUU KUSINI MBEYA.


Makamu Mwenyekiti wa mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Joseph Mapunda akisoma Hotuba kwa Waandishi wa Habari.

Mwanasheria Mkuu wa (TCRA) Ally Hassani Bwanga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)


Wahariri wa Vyombo Mbalimbali kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu kusini wakisikiliza



Baadhi ya Wahariri na wasimamizi wa Vipindi wa Vituo vya Nyanda za Juu Kusini wakifatilia Mjadala wa Maudhui ya Uandishi wa Habari na Utangazaji (Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)

Baadhi ya Wahariri na wasimamizi wa Vipindi wa Vituo vya Nyanda za Juu Kusini wakifatilia Mjadala wa Maudhui ya Uandishi wa Habari na Utangazaji (Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)







Waandishi wa habari nchini wameaswa kuzingatia maadili na kanuni za utangazaji kwa kuhakikisha kuwa wanaandaa vipindi bora ambavyo vina maslahi kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Joseph Mapunda katika warsha ya wahariri na waratibu wa vipindi vya Redio wa vyombo vya habari vya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayofanyika jijini Mbeya.

Mapunda amesema kuwa lengo kuu la Warsha hiyo ni kuelimishana na kukumbushana maudhui adilifu yenye kuelimisha na kuuburudisha umma wa Watanzania ili uweze kufahamu masuala mbalimbali yanayotokea katika jamii ikiwemo changamoto na jinsi ya kuzitatua.

Amesema tasnia ya habari kwa sasa inakabiliwa na chngamoto lukuki ikiwemo waandishi kutokuwa na weledi wa kutosha katika masuala mbalimbali yanayohusiana na mustakabali mzima wa taifa,huku akitoa wito kwa wanahabari kuangalia maslahi mapana ya Utaifa pindi wanapoandaa vipindi vyao.

Katika hatua nyingine Mapunda amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia kanuni na taratibu za uendeshaji wa vituo vyao vya radio kulingana na jinsi walivyokubaliana wakati wakipewa leseni za urushaji wa matangazo.

0 Responses to “TCRA YAWANOA WAANDISHI WA HABARI WA NYANDA ZA JUU KUSINI MBEYA.”

Post a Comment

More to Read