Wednesday, September 21, 2016
MKUU WA MKOA WA MBEYA ATANGAZA VITA NA MAJAMBAZI AWAOMBA WANANCHI USHIRIKIANO
Do you like this story?
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola hususani jeshi la polisi katika operesheni YA dhibiti ujambazi Mkoa wa Mbeya ili Mkoa huo uendelee kuwa salama na wananchi wawe salama na mali zao.
Hayo ameyasema leo ktk mkutano wa hadhara mjini Chunya alipokuwa akisikiliza Kero za wananchi na kuwaonya majambazi popote yalipo yasipange Mipango ya kufika ktk Mkoa huo.
Amesema jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya nimefanya kazi kuwa YA kudhibiti ujambazi na hivi karibuni limekamata majambazi yalikuwa yakitafutwa kutoka Mikoa ya Tanga na Mbeya na hata yaliyojaribu kufanya uhalifu wilaya yachunya yote yalinyanganywa silaha Haraka
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kuyafichua majambazi.
Aidha kwa taarifa alizonazo Wilaya ya Chunya ni wilaya inayomezewa mate na majambazi kutokana na shughuli za madini hivyo ni vema tukatoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi kudhibiti njama, mipango na matukio ya ujambazi
Amewahakikishia wananchi kuwa serikali ya mkoa chini ya uongozi wake hawatakubali majambazi kutamba na kufanya matukio bali wamejipanga kuona Mkoa unaendelea kuwa shwari na hao majambazi wautangaze Mkoa wa Mbeya kuwa si mkoa rafiki kwao na Amewataka polisi kuwa imara na akawasisitiza kwa kauli "WAKIJA NA MOTO NENDENI NA MOTO hakuna diplomasia katika kupambana na Jambazi"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA ATANGAZA VITA NA MAJAMBAZI AWAOMBA WANANCHI USHIRIKIANO”
Post a Comment