Wednesday, September 21, 2016

PEP GUARDIOLA HAPENDI WACHEZAJI WENYE MAUMBO MAKUBWA; MENEJA WA YAYA TOURE





Mahusiano kati ya mchezaji Yaya Toure ma Kocha wa Man City yanaendelea kuwa mabaya zaidi baada ya wakala wa Yaya Toure Dimitri Seluk kusema kocha huyo hapendi wachezaji wenye maumbo makubwa. Kabla ya Toure ikumbukwe kuwa Pep pia hakupatana kabisa na Ibrahimovic wakati akiwa Barcelona. Pep amesema hata mpanga kabisa Yaya Toure baada ya kumkosoa kwa kutokumweka kwenye list ya wachezaji wa kucheza.




Pep Ametoa sharti moja kwa Yaya Kuweza kucheza kwa kusema kuwa kwanza wakala wake Dimitri Seluk aende kwenye vyombo vya habari na kuomba msamaha kwa klabu ya Man City pamoja na wapenzi na mashabiki wake.
Akiongea na Sky Sports Dimitri Seluk alijibu kuwa kama kweli Pep anataka yeye aombe msamaha basi kwanza Pep aanze yeye kuomba msamaha kwa Pellegrini kwa alichomfanyia.



Alipouliwa tena kama ataomba msamaha Seluk alisema "sawa, niombe msamaha kwa kitu gani ? Kama Pep anaitaka vita, sawa anaweza”.
"Amekuja juu kwa nilichokisema kuhusu yeye kumuadhibu Yaya tena. lakini sijashangazwa. Pep hataki wachezaji wenye nafasi kubwa. Anataka wachezaji wanaomuogopa na watafanya kila atakachosema” alimalizia Wakala wa Yaya Dimitri Seluk”
 



0 Responses to “PEP GUARDIOLA HAPENDI WACHEZAJI WENYE MAUMBO MAKUBWA; MENEJA WA YAYA TOURE”

Post a Comment

More to Read