Tuesday, September 20, 2016
MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE ARUSHA WANALIPWA
Do you like this story?
MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata |
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
…………………………………………………………………
MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo
amemuagiza mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia kulipa madeni yote
wanayodai walimu ya milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo
wamekuwa wakidai
serikali kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi .Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi.Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na kwamba hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu
ndio inayopaswa izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufundisha na kufuatilia kila siku madeni hayo.
“Mkurugenzi nakupa muda wa wiki
mbili deni hili la milioni 154 kwa ajili ya walimu akikisha zinalipwa haraka
iwezekanavyo wakishalipwa ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa
kwani haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku
wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji
hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa
fedha hizo ambazo ni madeni hayo zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba
atahakikisha kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani
za halamshauri hiyo ili zikija zirejeshwe.
Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka
kwenye fedha alizoziokoa ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa
madiwani ambapo kiasi cha milioni 130 zilizokuwa
zinatumika kuwalipia madiwani mafuta ,simu pamoja na nauli
zitaelekezwa kulipa walimu hao madai yao ili waweze kujikimu na hali
wanayokabiliana nayo.
‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya
mafuta ni milioni 40.8,fedha za simu za madiwani milioni 61.2,nauli
iliyookolewa milioni 28 ambapo jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume
hivyo fedha hizi zinaelekezwa kwa walimu wa msingi na sekondari ikiwa ni madeni
wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lakini tumeona
tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha watoto wetu
vizuri”alisema Kihamia .
Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha
hizo kwa walimu hao wakati wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili
waendelee kujikimu kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea
hivyo zitaongeza ufanisi kwa walimu katika kufundisha
wanafunzi na akili zao na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili
wapate elimu
bora.
bora.
Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao
walisema kuwa wanakabiliwa na tatizo la kutopandishwa madaraja kwa
waliokaa kazini muda mrefu huku wengine walioingia kazini muda
mfupi wakiwa wanapandishwa madaraja bila kujua vigezo hivvyo
kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE ARUSHA WANALIPWA”
Post a Comment