Tuesday, September 20, 2016
BAADHI YA MAENEO HALMASHAURI YA CHALINZE YAKABILIWA NA UHABA WA CHAKULA
Do you like this story?
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na viongozi mbalimbali wa serikali mkoa,wilaya pamoja na halmashauri mkoani humo juu ya hali ya chakula kimkoa.(Picha na Mwamvua Mwinyi) |
Na
Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI
mkoani Pwani imesema halmashauri ya Chalinze inakabiliwa na upungufu wa
chakula ambapo unahitaji tani 443 za chakula cha bure kwa ajili ya watu 8,491
kutoka kwenye kaya 1,698.
Aidha
imesema pia kunahitajika tani 1,404 za chakula cha bei nafuu kwa watu 26,889
kutoka kwenye kaya 5,378.
Mbali ya
hayo,baadhi ya vyakula vikuu vinavyopatikana sokoni kutoka mikoa mingine bei
zipo juu ikiwemo mahindi,sembe,mchele,maharage na sukari.
Akizungumzia
hali ya chakula katika msimu wa mwaka 2015/2016 na maandalizi ya kilimo kwa
msimu wa 2016/2017 ,kwa baadhi ya viongozi wa serikali mkoa,wakuu wa
wilaya,wabunge na wenyeviti wa halmashauri ,mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi
Evarist Ndikilo,alisema hali ya chakula kimkoa ni ya wastani.
Alisema
halmashauri ya Chalinze imekubwa na upungufu huo kwa sababu iliathirika zaidi
na uhaba wa mvua katika kipindi cha msimu uliopita.
Mhandisi
Ndikilo,alielezea kuwa tathmini ya kina ya hali ya chakula imefanywa na wataalamu
wa mkoa na kubaini upungufu huo wa tani 443 za chakula.
Alisema
mkakati ili kukabiliana na tatizo hilo, halmashauri zinapaswa kuwa na mazao ya
mkakati kulingana kiasi cha mvua ikiwa ni pamoja na Chalinze kutakiwa kutilia
mkazo mazao ya muhogo na mtama na kujiwekea kampeni maalum ya ondoa njaa
Chalinze(ONJACHA).
“Elimu
kwa wakulima iendelee pia kutolewa juu ya kutambua umuhimu wa utunzaji wa
chakula na kiasi cha chakula kinachohitajika katika kaya kwa mwaka mzima .Na
hii itasaidia kuondokana na upungufu wa chakula ‘alisema mhandisi Ndikilo.
Alieleza
kuna kila sababu ya watendaji wa vijiji kuhakikisha wanasimamia sheria ya nguvu
kazi kuona kwamba vijana na watu wenye nguvu wanajishughulisha na shughuli za
kilimo.
Mhandisi
Ndikilo alizitaka halmashauri ziendelee kuhamasisha wananchi kun’goa visiki ili
matrekta yatumike kikamilifu.
Alisema
halmashauri hizo zisimamie kila kaya kulima ekari moja ya muhogo kwani uzoefu
unaonyesha maeneo yanayozalisha muhogo kwa wingi hayakabiliwi na uhaba wa
chakula.
Alisema
ni matarajio yake endapo mikakati hiyo itazingatiwa na kusimamiwa kwenye msimu
ujao wa chakula hali itakuwa shwari.
Hata
hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema ,taratibu zinaendelea kufanyika ili kukabiliana
na tatizo hilo kupitia ngazi husika hadi ofisi ya waziri mkuu.
Nae afisa
tawala msaidizi uchumi na uzalishaji mkoani humo,Shangwe Twamala akizungumzia
suala la mfumuko wa bei za vyakula vikuu,alisema bei za sokoni hadi kufikia
agost mwaka huu mahindi yanauzwa kwa sh.1,000 .
Alisema
kwa upande wa sembe ni sh.1,200,mchele 1,300 hadi 1,900,maharage 2,000 hadi
2,200 na sukari ni sh.2,200 hadi 2,400.
Twamala
alisema utekelezaji na malengo msimu wa kilimo uliopita ,kilimo cha vuli na
masika hakikuwa kizuri kutokana na uchache wa mvua hali iliyosababisha mazao
kama mahindi kukauka licha ya hekta 154,100 zililimwa na kuzalisha tani 675,717
za chakula.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BAADHI YA MAENEO HALMASHAURI YA CHALINZE YAKABILIWA NA UHABA WA CHAKULA”
Post a Comment