Tuesday, September 20, 2016

PASTA AJINYONGA BAADA YA KUTUMA PICHA ZA SEHEMU ZAKE ZA SIRI KWENYE WHATSAPP GROUP LA KANISA




Pasta kutoka Abuja, Nigeria Pasta Letsego amechukua maamuzi ya Kujinyonga baada ya kutuma picha za sehemu zake za siri kwenye WhatsApp Group la Kanisa kimakosa ambapo alikuwa akimtumia hawara yake ambaye pia anasali kwenye kanisa hilo nchini Afrika Kusini.

Katika picha hizo alizotuma Pasta Letsego aliziambatanisha na ujumbe usemao “mke wangu hayupo, hii ni mali yako usiku wa leo”.  Baada ya kutuma picha hizo kimakosa katika group la kanisani, alijitoa mara moja kwenye group hilo na kuacha kupokea simu zote zilozokuwa zikipigwa kwenye simu yake.

Pasta Letsego alikutwa amefariki masaa 24 baada ya tukio hilo, akiwa amejinyonga ndani ya nyumba ambayo amepangishiwa na kanisa.
Pasta Letsego alikuwa akihubiri kanisa la Christ Embassy ambalo linamilikiwa na Pasta Chris Oyakhilome kutoka nchini Nigeria.

0 Responses to “PASTA AJINYONGA BAADA YA KUTUMA PICHA ZA SEHEMU ZAKE ZA SIRI KWENYE WHATSAPP GROUP LA KANISA”

Post a Comment

More to Read