Thursday, September 25, 2014
CHOMBO CHOCHOTE CHA HABARI KITAKACHO KIUKA MAADILI YA HABARI KUKIONA CHA MOTO
Do you like this story?
![]() |
Sehemu ya wafanyakazi wa Radio Triple A fm wakiwa katika picha ya pamoja
kulia na kushoto kwa naibu waziri Nkamia ni Meneja wa redio hiyo Fredy Mumburi kushoto ni mkurugenzi wa redio hiyo Papa king molel baada ya uzinduzi wa
logo ya redio hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki picha kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog |
![]() |
Baadhi ya viongozi wa serekali wa jiji la Arusha nao waliudhuria uzinduzi huo |
![]() |
Meya
wa Jiji la Arusha Gaudensi Lyimo akitoa nasaha chache kwa wageni
waliohudhuria uzinduzi huo kwenye ukumbi wa blue Frem uliopo kwenye
klabu ya usiku ya TRIPLE A NIGHTY CLUB ya jijini hapa |
Nembo ya
radio Triple A fm na kuwataka wamiliki na wanahabari kuhakikisha wanafuata
maadili ya taaluma ya uandishi wa habari iwe kazini au nje ya kazi zao.
Serikali imesisitiza kuwa haitavifumbia macho vyombo vya habari vitakavyo
kiuka maadili ya habari na kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali vyombo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari vijana utamaduni na
michezo Juma Nkamia wakati akizindua logo ya redio Triple A fm jijini hapa huku
akiwataka wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao iliwaweze kuitumikia jamii
bila ya kuleta uchochezi kwa jamii utakaopelekea uvunjifu wa amani.
Nkamia alisema kuwa Taaluma hiyo inaweza kuileta jamii katika kukabiliana
na mmomonyoko wa maadili uaoendelea hapa nchi au kuzidi kuumomonyoa maadili
hayo kwani wao kazi yao ni kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha jamii
inayovizunguka vyombo hivyo hivyo vinamchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.
"Lengo hapa ni kuhakikisha kuwa vymbo vya habari haviwi ndio
kichocheo cha uvunjifu wa amani ila nawasihi muwe kichocheo katika suala zima
la kupiga vita mmomonyoko wa maadili yetu kwa nyinyi mpo karibu zaidi na
jamii"alisisitiza Nkamia
Kwa Upande wake Meneja wa Tcra kanda ya kaskazini Anethy Matindi
aliwakemea mablogger kwa kupachika picha zinazo vunja sheria za nchi ikiwemo
pia kupachika picha zisizofaa kwa jamii na kuwa dawa yao ipo inakuja
Matindi alisema kuwa imekuwa ni tabia kwa vyombo vya habari kutofuata
maadili hivyo akavitaka kuacha mara moja kutumia vyombo hivyo kwa kukiuka
taaluma na weledi wa tasnia hiyo
Naye meya wa jiji la Arusha Gaudency Lyimo alisema kuwa anaipongeza
Triple A Fm kwa kuweza kusogeza habari kwa jamii ya wakazi wa jiji la Arusha
ambapo taarifa zimekuwa zikifika kwa wakti hivyo kuchangia kukua kwa sekta
mbali mbali na kuleta maendeleo kwa jamii
Mkurugenzi wa The Blue Triple A Ltd Papaa King
aliwashukuru viongozi wote waliohudhuria katika uzinduzi huo huku akitabaisha
kuwa Redio hiyo itafuata taratibu zote za kisheria katika kujiendesha ikiwemo
kuwapa maslahi mazuri wafanyakazi wake iendane na viwango .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CHOMBO CHOCHOTE CHA HABARI KITAKACHO KIUKA MAADILI YA HABARI KUKIONA CHA MOTO ”
Post a Comment