Friday, August 12, 2016
Rais Magufuli Akerwa na Uozo Uliopo Ndani ya CCM.......Aagiza Jiji la Mwanza Lisiwatoze Kodi Wafanyabiashara Wadogowadogo
Do you like this story?
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuna mambo ya hovyo ambayo yapo ndani ya Chama
cha Mapinduzi ambayo yanahitaji kuhojiwa na kupatiwa majibu yenye tija.
Aikihutubia
maelfu ya wananchi jana waliojitokeza kumsikiliza katika viwanja vya Furahisha
Jijini Mwanza Dkt. Magufuli alisema anafahamu kwamba ndani ya CCM kuna mambo ya
hovyo na mfano ni uwanja wa CCM Kirumba na majengo mengine ya CCM ambayo
ukiuliza maduka na ofisi zinazozunguka majengo hayo mapato yake yako wapi
huwezi kupata majibu ya kuridhisha.
"Ninyi
wananchi wa Mwanza na wanachama wa CCM hojini haya na atakayewauliza mwambieni
ni mimi Mwenyekiti wa CCM nimesema muwaulize, nataka chama ambacho mali zake
zinajulikana kwa sababu ukienda kuwauliza mnakusanya shilingi ngapi kwa chumba
kimoja wanaweza kukuambia ni elfu 50 kumbe wanaingiza laki 5" Alisema Rais Dkt. Magufuli
Rais
Magufuli alisisitiza kwamba anaitaka CCM ya Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl.
Julius Nyerere siyo CCM ya watu ambao mchana wapo CCM na usiku wapo vyama
vingine, wanaofanya hivyo ni bora wahamie huko moja kwa moja.
Aidha
katika hatua nyingine Rais Dkt. Magufuli ameagiza uongozi wa Jiji la Mwanza
kutowatoza ushuru wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuwa wanatakiwa wanufaike na
taifa lao na pia wamachinga waachwe mjini kwanza hadi hapo watakapo andaliwa
mazingira mazuri ya kufanyia biashara yatakayokuwa na wateja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Rais Magufuli Akerwa na Uozo Uliopo Ndani ya CCM.......Aagiza Jiji la Mwanza Lisiwatoze Kodi Wafanyabiashara Wadogowadogo ”
Post a Comment