Thursday, September 22, 2016

ULEVI WAMKOSESHA DILI ADEBAYOR KUJIUNGANA LYON





Emmanuel Adebayor ameshindwa kufanikisha lengo lake la kujiunga na klabu ya Lyon baada ya kuvuta sigara na kunjwa wakati akiwa bado kwenye mahojiano na Boss wa klabu ya Lyon.

Akiwa kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Crystal Palace kuisha kipindi cha Kiangazi, bado ameshindwa kufanikisha nia yake kujiunga na klabu hiyo ya Lyon kwa kosa la kunywa akiwa kwenye interview na Boss wa klabu ya Lyon Mr. Bruno Genesio.

Kulikuwa na nafasi kwenye Kikosi chetu ya Lyon ambayo tulidhani Adebayor angeweza kuichukua, nilipanga kukutana nae, lakini cha kunishangaza ni alipofika akaomba kikombe chake cha kahawa kiwekwe Whisky huku akiwa na sigara mdomoni kwake. Hapo ndipo nilipojua kuwa hakuna nafasi yake kwenye Kikosi chetu alisema Rais wa klabu ya Lyon Mr. Bruno Genesio.

Adebayor kwa sasa amekuwa akihangaka kutafuta timu gani anayoweza kwenda kuichezea ili kuendeleza kipaji chake, ambapo siku za hivi karibuni kulikuwa na uvumi wa yeye kurudi kwenye klabu yake ya Zamani Toottenham.

0 Responses to “ULEVI WAMKOSESHA DILI ADEBAYOR KUJIUNGANA LYON”

Post a Comment

More to Read