Friday, October 21, 2016
ALICHOKISEMA RAIS MAGUFULI KUHUSU MIKOPO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU
Do you like this story?
Rais
wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 483
kwa mwaka huu kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu ambapo wanafunzi zaidi ya
118,000 watanufaika.
Akizungumza
katika uwekaji wa jiwe la msingi la hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo,
Rais Magufuli amesema miongoni mwa hao watakaonufaika, wanafunzi 93,000 ni
wanaoendelea na masomo na wanafunzi takribani 25,000 ni watakaoanza masomo
mwaka huu huku akiweka bayana kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa wanafunzi ambao
wanatoka kwenye familia masikini.
Rais
Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kurekebisha dosari
zilizopo katika mfumo wa utoaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na upangaji mbaya wa
wanafunzi katika vyuo, kutoa mikopo kwa upendeleo, kutozingatia sifa za
mkopaji, kutoa mikopo hewa na kufungua vyuo kabla ya mikopo ya wanafunzi
kutolewa na pia amewaonya wanafunzi kujiepusha na vitendo visivyofaa wakati
Serikali inarekebisha dosari hizo.
"Na
ndio maana wakati mwingine na wabaya wanapitia humo humo, mara fanye hivi
fanyeni vile, wakati wanajua kuwa mkifanya yasiyofaa Serikali itawafukuza tu
ili mkafanyie mambo yenu huko.
"Kwa
sababu huwezi kuwa unahangaika kutafuta fedha za kuwapa mikopo, wakati huo huo
unahitaji kujenga reli, wakati huo huo unahitaji kujenga barabara, wakati huo
huo unahitaji kulipa mishahara, wakati huo huo unahitaji kutoa elimu bure,
wakati huo huo Karagwe kuna njaa, wakati huo huo watu wanahitaji dawa
hospitali, halafu watu wengine wanataka kukuendesha kana kwamba hela
unayokusanya ni kwa ajili yao tu, ni lazima tuelewane na mimi ninataka
kuwaeleza kwa dhati lazima twende katika njia iliyonyooka, ni bora uwe Rais
usiye maarufu lakini utimize uliyoyaahidi, asitokee mtu wa kukuendesha, ninajua
mmenielewa" amesisitiza Dkt.
Magufuli.
Dkt.
Magufuli ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kujipanga vizuri
kukusanya marejesho ya mikopo kwa wote waliokopeshwa na bodi hiyo ambapo mpaka
sasa bodi inadai takribani Shilingi Trilioni 2.6.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ALICHOKISEMA RAIS MAGUFULI KUHUSU MIKOPO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU”
Post a Comment