Tuesday, November 22, 2016
BABA AMBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA 3 MPAKA KUFARIKI DUNIA
Do you like this story?
Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka
mitatu mkazi wa Kijiji cha Nyamihaga Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma amekufa
baada ya kunajisiwa na baba yake wa kambo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma,
Ferdinand Mtui alisema jana kwamba wamemtia mbaroni mtuhumiwa Hamimu Saidi (27)
mkazi wa kijiji hicho cha Nyamihaga.
Akitoa maelekezo kuhusu mkasa huo,
Kamanda Mtui alisema mtuhumiwa alitekeleza dhamira yake hiyo wakati mama wa
mtoto huyo ambaye alikuwa mke wa mtuhumiwa alipokwenda kisimani kuchota maji.
Alisema baada ya mwanamke huyo kurejea
nyumbani kutoka kisimani alimshuhudia mtoto wake akilalamika sana wakati
akitaka kujisaidia haja ndogo na ndipo alipomchunguza akagundua kwamba mtoto
huyo alikuwa ameingiliwa na kujeruhiwa kwenye sehemu zake za siri.
Kamanda Mtui alisema baada ya kugundua
hilo, mama huyo wa mtoto alimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitali ya Mkoa
ya Maweni kwa matibabu, ambako iligunduliwa kuwa mtoto huyo alikuwa amenajisiwa
na alikuwa amebanwa shingo wakati akifanyiwa kitendo hicho hivyo alikosa pumzi
wakati akifanyiwa unyama huo.
Kamanda huyo alisema hata hivyo mtoto
huyo alifariki katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni alipokuwa akitibiwa na kwamba
baada ya uchunguzi wa kidaktari na uchunguzi wa Polisi, mwili wa mtoto huyo
ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.
“Kwa sasa mtuhumiwa Hamimu
Saidi anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Kigoma wakati upelelezi
ukiendelea ili taratibu za kumfikisha mahakamani zifanyike na kwamba anatarajia
kufikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi huo utakapokamilika,” alieleza Kamanda
Mtui.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BABA AMBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA 3 MPAKA KUFARIKI DUNIA”
Post a Comment