Thursday, November 17, 2016
GARI LA WIZI LAMPONZA PADRI WA KANISA KATOLIKI SUMBAWANGA
Do you like this story?
Kikosi
Kazi cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam cha kuzuia wizi wa magari
kimeendelea na kazi ya kudhibiti vitendo hivyo kwa kumkamata Padri wa Kanisa
Katoliki Sumbawanga Demestrious Apolinary kwa tuhuma za kuhusika na ununuzi wa
gari ya wizi.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro amesema mnamo
Novemba, 11 baada ya padri huyo kununua gari aina ya Toyota L/cruiser T616 DCH
mali ya Joseph Kayawaya lililoripotiwa kuibiwa Dar es Salaam na nyaraka za
kughushi na kuuzwa jijini Arusha.
Amesema
padri huyo anafanyiwa mahojiano na kwamba upelelezi utakapokamilika atapelekwa
mahakamani ili kuona kama ni mnunuzi asiye na hatia au alishiriki kwa namna
moja au nyingine katika wizi huo.
Kamanda
Sirro amesema pia Jeshi la Polisi linashikilia watuhumiwa wengine wanne
aliowataja kwa majina ya Aman Dickson, Exaud Martin, Rashid Haruna na Mzee
Nasibu kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa magari katika matukio mawili tofauti.
Katika
tukio lingine, Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi linashikilia majambazi
watano na vifaa mbalimbali walivyopora maeneo ya Tuwangoma mtaa wa Masaki,
Mbagala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ GARI LA WIZI LAMPONZA PADRI WA KANISA KATOLIKI SUMBAWANGA”
Post a Comment