Wednesday, November 16, 2016
SPIKA JOB NDUGAI AKILI KUWEPO KWA CHANGAMOTO NYINGI BUNGENI
Do you like this story?
Spika
wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai amekiri uwepo wa
wabunge wapya kwenye bunge la 11 ambao ni asilimia 70 ya wabunge wote ni
changamoto kubwa katika uendeshaji wa vikao vya muhimili huo kwani wengi wao
bado hawajui majukumu yao kutokana na kutozifahamu kanuni.
Mhe
Ndugai anabainisha changamoto hiyo mbele ya wajumbe kutoka nchi za jumuiya ya
Nordic pamoja na washirika wa maendeleo kutoka shirika la maendeleo la umoja wa
mataifa (UNDP) ambao ni wafadhili wa mradi wa kuwajengea uwezo wabunge na
watumishi walipomtembelea ofisini kwake ambapo amesema wabunge wapya wanahitaji
mafunzo ya kina kuhusu masuala ya kibunge.
Kwa
upande wake mkuu wa msafara wa wajumbe hao ambaye ni muwakilishi wa UNDP nchini
Alvaro Rodriguez amesema pamoja na mambo mengine ujumbe huo unaamini kupitia
bunge la Tanzania itafikia malengo yake endelevu ifikapo mwaka 2030 huku
wakipongeza mpango wa Tanzania wa kutaka kuwa na asilimia 50 kwa 50 ya wabunge
wanaume na wanawake.
Aidha
ujumbe huo pia ukatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo chini ya ufadhiliwa
na UNDP pamoja na wajasiriamali ikiwemo wasindikaji wa mafuta ya alizeti kanda
ya kati ambao wameomba serikali na wahisani hao kuangalia namna ya kuongeza
thamani ya bidhaa hiyo ili iweze kumudu soko la ushindani la ndani na nje ya
nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SPIKA JOB NDUGAI AKILI KUWEPO KWA CHANGAMOTO NYINGI BUNGENI”
Post a Comment