Saturday, May 17, 2014
TAARIFA ZA AWALI KUHUSU KIFO CHA ADAM KUAMBIANA.
Do you like this story?
Marehemu Adam Kuambiana akiwa location enzi za uhai wake. |
Hizi
ni taarifa zingine za ghafla ambazo Tanzania tumezipokea kwa mshtuko na
masikitiko ni kifo cha miongoni mwa-madirector wa Tanzania ambao ni waigizaji
pia,huyu ni Adam Kuambiana ambaye taarifa za kifo chake zimeanza kusambaa
mchana wa Mei 17.
Mwenyekiti
wa Bongo Movie Steve Nyerere amesema>>’Mwenzetu Adam Philipo Kuambiana
amefariki akiwa Location ana shoot,mimi nimepigiwa simu saa 3 asubuhi kuwa
hospitali pale Mwenge niende nikahakikishe kuwa ni kweli Adam amefariki na
kweli kufika pale nikamkuta Adam Kuambiana amefariki’
‘Sasa
hivi tumetoka Muhumbili kwenda kumsitiri mwenzetu,taarifa inasema wakati yupo
location alikua analalamika tumbo linamuuma linamuuma kumfikisha hospitali
ndipo umauti ukamfika’.
Kwa
mujibu wa Steve Nyerere amesema kuwa marehemu Adam kuambiana alikua ana shoot
filamu yake mpya ambayo ndani yake amewashirikisha wasanii kadhaa wa Bongo
fleva akiwemo Q Chillah,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA ZA AWALI KUHUSU KIFO CHA ADAM KUAMBIANA.”
Post a Comment