Monday, November 14, 2016
HATIMA YA DHAMANA KESI YA GODBLESS LEMA KUJULIKANA LEO
Do you like this story?
Wakati
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema (40) akitarajia kujua hatima ya
dhamana yake katika Mahakama Kuu leo, kesho yeye na mkewe Neema Lema (33)
watapanda kizimbani kwa kesi ya uchochezi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo.
Ijumaa
iliyopita Lema alipelekwa Gereza la Kisongo, Arusha baada ya kunyimwa dhamana
katika kesi nyingine ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli,
hatua ambayo imepingwa na chama chake na mawakili wake.
Katibu
wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist Lazaro alisema hawakuridhishwa na pingamizi
la dhamana lililowekwa na mawakili wa Serikali kwani tayari Lema alikuwa
amepewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi.
“Tayari
tumefanya mazungumzo kuongeza nguvu za mawakili wa chama ambao wataungana na
mawakili wa Arusha kudai dhamana leo,”
alisema.
Mmoja
wa mawakili hao, Shaki Mfinanga alisema leo wanatarajia kuwasilisha maombi ya
dhamana ya Lema wakiwa na mawakili wa Chadema.
Kesi
ya mkewe
Wakati
hayo yakiendelea, kesho Lema na mkewe watakuwa mahakamani mbele ya kaimu Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mkoa Arusha, Desdery Kamugisha.
Katika
kesi hiyo, Hakimu Kamugisha amewapa dhamana washtakiwa hao katika kesi ya
kusambaza ujumbe kumkashifu mkuu wa Mkoa Arusha.
Lema
anadaiwa kuwa Agosti 20, 2016 akitumia simu namba 076415**47 ambayo imesajiliwa
kwa jina la mkewe, alituma ujumbe kwenye namba ya Gambo 0766 75**75 wenye
maneno ya uchochezi.
Maneno
hayo; “Karibu Tutakudhibiti kama Uarabuni walivyodhibiti Mashoga”
yanadaiwa ya uchochezi kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Adhabu, Kifungu cha
118 (a) na Kifungu cha tatu katika sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.
Katika
shtaka jingine, Lema anashtakiwa peke yake, akituhumiwa kivunja Sheria ya
Makosa ya Jinai namba 390 kifungu cha 35 kwa kuhamasisha maandamano kinyume cha
sheria wakati wa mkakati ulioitwa Ukuta na chama hicho.
Lema
alidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti Mosi hadi 26 kwa kusambaza ujumbe
kupitia mtandao wa WhatsApp wakati akijua kufanya ni kosa kisheria. Katika kesi
hiyo, Lema na mkewe wanatetewa mawakili wanne, John Mallya, James Lyatuu,
Reygod Nkya na Mfinanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ HATIMA YA DHAMANA KESI YA GODBLESS LEMA KUJULIKANA LEO”
Post a Comment