Monday, November 14, 2016

KUNDI LA MIFUGO LAPELEKEA MAUAJI MKOANI RUKWA




Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mfugaji Sandu Mwandu, ameuawa kikatili na kundi la watu wenye hasira kali wa kijiji cha Kifone katika kata ya Mwimbi, wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, baada ya kutokea kutoelewana kati ya wakulima na wafugaji, kufuatia kundi la Ng’ombe kuachiliwa kuingia kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu kiasi kikubwa cha mazao.

Baadhi ya mashuhuda wakielezea sakata hilo kwenye maeneo ya kijiji hicho, akiwemo na diwani wa kata ya Mwimbi Bw Claudio Mweupe, wamesema licha ya mfugaji huyo kuuawa kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga, lakini na mwenziwe naye Rehi Mwandu amejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na kundi hilo la wakulima, na hivi sasa amelazwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga, huku msako mkali ukiendelea kuwatafuta watu wote waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mkononi.

Mkuu wa wilaya ya Kalambo Bi Julieth Binyura, akiongea kwenye kijiji hicho cha Kifone akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa chini ya mwenyekiti wake Bw Zelote Steven, amesema tayari wameanza kuwashikilia viongozi wa vijiji na vitongoji wanaoruhusu makundi ya Ng’ombe kuingia kwenye maeneo yao kinyemela, kwani imeonesha ndio kitendo kinachochangia kusababisha migogoro ya ardhi wilayani humo.

0 Responses to “KUNDI LA MIFUGO LAPELEKEA MAUAJI MKOANI RUKWA”

Post a Comment

More to Read