Thursday, November 17, 2016
LIPUMBA ATISHIA KUMPIGA MARUFUKU MAALIM SEIF KUFANYA MIKUTANO TANZANIA BARA
Do you like this story?
Mwenyekiti
wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema atampiga marufuku Katibu
Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kufanya mikutano ya kisiasa
Tanzania Bara kama hatamtambua kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho.
Lipumba
alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi wa CUF kwenye mkutano wa
ndani mkoani Geita.
Ziara
ya Lipumba imefanyika wakati Maalim Seif akiwa amesambaza barua kwa viongozi wa
CUF wa wilaya zote nchini akiwataka wasishirikiane na Profesa Lipumba huku
akionya atakayekaidi atachukuliwa hatua.
“Kama
Maalim Seif hatambui kuwa mimi ni mwenyekiti wake, huku mimi nikimtambua kuwa
Katibu Mkuu wangu, basi naye tutamzuia kufanya mikutano ya kisiasa Tanzania
Bara,” alisema Lipumba.
Profesa
Lipumba alisema hana tatizo na wananchi wa Zanzibar wala kiongozi wa upinzani
atakayetetea watu hao na kuongeza kuwa yeye amekuwa mstari wa mbele kutetea
Wazanzibari.
“Mimi
natambua kuwa ndiye mwenyekiti halali wa chama hiki na mwenye mamlaka ya
kumwondoa mwenyekiti au katibu ni mkutano mkuu wa chama na lazima theluthi moja
ya wajumbe watoke Bara na theluthi nyingine Zanzibar, lakini mkutano huo
haukufanyika wala muhtasari haupo,” alisema
Profesa Lipumba.
Alieleza
kwamba kwa sasa yeye na wana CUF wengine wamejipanga kukijenga chama hicho.
Mwenyekiti
huyo pia alizungumzia suala la Muungano akisema ni muhimu kwa usalama wa nchi
na Taifa kwa ujumla.
Alisema
ili kulinda Muungano kuna mahitaji muhimu ya kuwa na vyama vyenye nguvu
vitakavyokuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi wa pande hizo
mbili.
Lipumba
alisema amefika wilayani hapa akitoka Urambo kwenye msiba wa Spika wa Bunge la
Tisa, marehemu Samuel Sitta ambapo pia aliongea na baadhi ya viongozi wa chama
hicho.
“Tumeifika
Kahama kuzungumza na viongozi wa hapa na wa wilaya jirani, dunia ina changamoto
kubwa katika masuala ya demokrasia na kujenga utawala bora kwa baadhi ya
viongozi,” alisema Lipumba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ LIPUMBA ATISHIA KUMPIGA MARUFUKU MAALIM SEIF KUFANYA MIKUTANO TANZANIA BARA”
Post a Comment