Wednesday, November 23, 2016
MIKOA INAYOONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI NCHINI TANZANIA
Do you like this story?
Mikoa ya Tabora, Katavi na Rukwa imetajwa kuwa ni miongoni
mwa mikoa 10 inayoongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 za Taasisi
ya Mkapa.
Taarifa hiyo iliyotlewa na Meneja Mradi wa TB na Ukimwi
kutoka Taasisi ya Mkapa, Dkt. Happenes Wilbroad katika
mafunzo ya siku moja ya viongozi wa dini yaliyofanyika
Nzega.
Alisema mkoa unaoongoza kwa maambukizi ya VVU kati ya mikoa
hiyo mitatu ni Rukwa wenyeasilimia 6.2 ukifuatiwa na Katavi
asilimia 5.2 na Tabora asilimia 5.1.
Dk. Wilbroad alisema Taasisi ya Mkapa imeanza kuendesha
mafunzo ya kuhakikisha wananchi wanatambua na kuepuka maambukizi mapya.
Alisema jitiahada mbalimbali za kudhibiti
maambukizi hayo zinapaswa kufanyika kunusuru maisha ya wakazi
wa maeneo hayo.
Alitaja sababu zinazochangia maambukizi kuwa ni pamoja
na ndoa za utotoni, tohara za jadi na baadhi ya wananchi kutozingatia elimu ya
Ukimwi na kukithiri imani potofu za ushirikina.
Wakizungumza baada ya mafunzo hayo, baadhi ya viongozi wa
dini walisema watahakikisha wanashirikiana na serikali kwa kutoa elimu kwa
jamii dhidi ya mapambano ya Ukimwi.
Mussa kassimu, Sheikh wa mjini Nzega
alisema elimu waliyopewa na wataalamu wa mafunzo hayo inalenga maagizo ya
imani zao za dini hasa katika kukemea jamii dhidi ya mambo maovu.
Mchungaji wa Kanisa la AICT, Isaya lyaka, AICT
alisema vitabu vya dini vinasema kila mmoja awe mwaminifu kwa mwenziwe
waliofunga ndoa na kwa wale ambao bado wanapaswa kusubiri.
– Mtanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MIKOA INAYOONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI NCHINI TANZANIA”
Post a Comment