Sunday, November 13, 2016

SERIKALI YAFUTA MIKOPO YA ELIMU KWA WANAFUNZI WA SERIKALI




Bodi ya mikopo ya elimu ya Zanzibar imefuta huduma za mikopo ya elimu kwa wafanyakazi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwataka wafanyakazi wachukue mikopo kutoka kwa waajiri wao.

Hatua hiyo imetangazwa na waziri wa elimu wa Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya wizara kuelezea hatua zilizochukuliwa baada ya serikali kuzuia mikopo hiyo kutokana na kuwepo malalamiko ya wanafunzi kukosa mikopo ambapo waziri amesema serikali imegundua kuwepo mikopo mingi kwa wafanyakazi hali inayosababisha wanafunzi kukosa huduma hiyo hivyo kuanzia sasa wafanyakazi wa wizara watalipiwa na wizara zao au kuchukua mikopo benki.

katika hatua nyengine waziri wa elimu amesema bodi hiyo ya mikopo  ya elimu itawasimamia kwa kuwalipia ada zote za amsomo katika vyuo vikuu hapa nchini wanafunzi kumi kati ya 50 waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita hiyo ikiwa ni ahadi ya rais wa Zanzibar Dr Ali Mohameds Shein aliyoitoa wakati alipokutana na wanafunzi hao ambapo amesema hatua hiyo itakuwa kila mwaka ili kuleta motisha kwa wanafunzi wa Zanzibar.

Mwezi uliopita rais wa Zanzibar Dr Shein alisitisha utoaji mikopo ya elimu na kutaka wizara na bodi kuangalia na kuunda mikakati mipya ili kuondosha lawama kwa wanafunzi wanaokosa mikopo hiyo ambapo   bodi hiyo katika maombi 2624 wameyapitisha maombi ya wanafunzi 372 watakaopatiwa mikopo ya elimu kwa mwaka 2016/2017.

0 Responses to “SERIKALI YAFUTA MIKOPO YA ELIMU KWA WANAFUNZI WA SERIKALI”

Post a Comment

More to Read