Tuesday, November 15, 2016
WANAFUNZI WAKUMBWA NA UGONJWA WA KUANGUKA
Do you like this story?
Wanafunzi
wa kike 12 wanaosoma Shule ya Msingi Nditi, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi,
wamekumbwa na ugonjwa wa kuanguka ghafla na wengine kupoteza fahamu, walipokuwa
wakicheza katika viwanja vya shule hiyo.
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Amon Livigha, alikiri kutokea tukio hilo katikati ya wiki
iliyopita, saa mbili asubuhi.
Alisema
baada ya tukio hilo, baadhi ya wazazi walifika shuleni hapo na kuwachukua
watoto wao na kwenda nao nyumbani.
“Nilipata
taarifa ya kuanguka kwa wanafunzi hao nikiwa darasani nafundisha, hivyo
kutokana na uzito wa tatizo, nililazimika kukatisha masomo na kwenda
kuwahudumia watoto hao.
“Wakati
tukiendelea kufanya utaratibu wa kuwakimbiza wanafunzi hao kituo cha afya
kupatiwa huduma, baadhi ya wazazi walikataa watoto wao wasipelekwe hospitali na
kuondoka nao,” alisema.
Mwalimu
Livigha alisema kutokana na tukio hilo, kamati ya shule, wazazi na uongozi wa
Serikali ya kijiji na kata hiyo wamekutana kujadili suala hilo.
Mtendaji
wa kata hiyo, Juma Mng’anga, alikiri kutokea tukio hilo na kueleza kuwa tayari
wameshatoa taarifa makao makuu ya wilaya, Nachingwea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI WAKUMBWA NA UGONJWA WA KUANGUKA”
Post a Comment