Thursday, February 23, 2017

BROWN IDEYE AONGEZA IDADI YA WAAFRIKA WANAOCHEZA SOKA CHINA


Mshambuliaji kutoka nchini Nigeria Brown Ideye ameongeza idadi ya waafrika wanaocheza soka nchini China, baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Tianjin Teda.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ameelekea mashariki ya mbali, akitokea nchini Ugiriki alipokua akiitumikia klabu ya Olympiakos.
Ideye amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu yake mpya huko China, na anaungana na mchezaji mwezake kutoka Nigeria John Mikel Obi na  Malick Evouna raia wa Gabon ambao walisajiliwa na Tianjin Teda mwezi uliopita.
Ideye anaondoka Olympiakos baada ya kucheza michezo 65 na kufunga mabao 28, na mwaka jana alichangia kwa kiasi kikubwa kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ugiriki.
Ideye alielekea nchini Ugiriki mwezi Agosti mwaka 2015 akitokea England kwenye klabu ya West Bromwich Albion.

Klabu ya Tianjin Teda ilimaliza msimu uliopita ikiwa kwenye nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini China, na usajili wa wachezaji hao kutoka Afrika unaaminika huenda ukasaidia kuongeza chachu ya ushindani msimu huu.

0 Responses to “BROWN IDEYE AONGEZA IDADI YA WAAFRIKA WANAOCHEZA SOKA CHINA”

Post a Comment

More to Read