Thursday, March 17, 2016

SUGU AONYESHA MAANDALIZI YA UJENZI WA HOTEL YAKE YA NYOTA TATU. MBEYA


Mwonekano wa  hoteli ya Sugu itakavyokuwa jijini Mbeya.

Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co Ltd, Mr Joseph Mbilinyi na Eng. Chao Nan wa kampuni ya ukandarasi Home Africa Investment Co Ltd ya China wakisaini mkataba wa ujenzi.



Msanii mkongwe wa Hip Hop na mbunge wa Mbeya mjini, Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameachia wimbo wake mpya ‘Freedom’ ambapo ndani ya wimbo huo amezungumzia mambo mbalimbali yakiwemo mafanikio yake.

Katika kibao hicho kilichoandaliwa katika studio za MJ Record chini ya producer Marco Chali, Sugu ameelezea jinsi alivyoweza kupambana mpaka kufanikiwa huku alionyesha zaidi kumshukuru mama yake.

Katika ‘Verse’ ya pili ya wimbo huo, Sugu amesema “Mama Hemedy mwanao nimefika mbali, maisha yana afadhali nakomaa ili nisifeli, kiukweli hata mwenyewe najikubali najenga mpaka hoteli?,” .

Pia hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa instagram alipost picha ya ujenzi wa hoteli hilo na kuandika: Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co Ltd Mr Joseph Mbilinyi na Eng. Chao Nan wa kampuni ya ukandarasi Home Africa Investment Co Ltd ya China wakisaini mkataba wa ujenzi. Kampuni hiyo itajenga hotel ya nyota 3 itakayoitwa Hotel Desderia jijini Mbeya na ujenzi unaanza mara moja kwa mkopo wa bank ya CRDB.

Katika post nyingine ya hivi karibuni aliandika: Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co. Ltd ya jijini Mbeya Joseph Mbilinyi akiwa kwenye makabidhiano ya site na wakandarasi wa Home Africa Investment Corp Ltd ya China… Mchakato wa ujenzi wa hotel hiyo ya nyota 3 umeanza rasmi leo… Mungu aendelee kubariki. Amen.

0 Responses to “ SUGU AONYESHA MAANDALIZI YA UJENZI WA HOTEL YAKE YA NYOTA TATU. MBEYA”

Post a Comment

More to Read