Saturday, March 19, 2016

NDEGE YA FLY DUBAI YAANGUKA NA KUUA 62


FlyDubai Boeing 737 -800

Ndege hiyo ilivyowaka moto.

Waliopoteza ndugu zao kwenye ajali hiyo wakiomboleza.



WATU 62 wamepoteza maisha dunia baada ya ndege ya FlyDubai Boeing 737 -800 kupata ajali wakati ikijaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Rostov-on-Don nchini Urusi usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hiyo, FlyDubai Boeing 737 -800 hufanya safari zake kati ya Dubai na Rostov-on-Don ilikuwa imetoka Dubai na kupewa flight namba FZ981, na kwamba hali ya hewa ilibadilika ghafla mita chache kabla ya kutua uwanjani hapo ndipo rubani akajaribu kutua umbali wa mita 100 kutoka uwanja wa Rostov-on-Don uliopo Jimbo la Rostov.

Inasemekana kuwa, ndege hiyo ilizunguka kwa takribani saa mbili kabla ya kufanya jaribio la pili la kutua mita 100 kutoka uwanjani hapo kufuatia hali mbaya ya hewa eneo la uwanja. Taarifa zimeongeza kuwa baada ya kuanguka ndege hiyo ilivunjika na kushika moto papo hapo.

Waliokufa kwenye ajali hiyo ni abiria 55 na wahudumu 7 wa ndege hiyo wakiwemo marubani. Aidha inasemekana hakuna aliyeokolewa na kwamba wote waliokuwemo wamepoteza maisha.

0 Responses to “ NDEGE YA FLY DUBAI YAANGUKA NA KUUA 62”

Post a Comment

More to Read