Thursday, March 17, 2016
MKUU WA MKOA WA MBEYA, AMOS MAKALA, ATOA MAAGIZO MANNE MAZITO KWA WATUMISHI WA SERIKALI.
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala
akizungumza na watumishi waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi na
Mkuu wa Mkoa mstaafu Abaas Kandoro Machi 17 mwaka huu.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)
|
Watumishi wa Serikali wakisikiliza kwa makini maagizo ya
Mkuu wa Mkoa huo Amos Makala wakati
akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abasi
Kandoro Machi 17 mwaka huu
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mstaafu Abasi
Kandoro (kulia) akimkabidhi rasmi ofisi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala
katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Machi 17
mwaka huu.
|
Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abas Kandoro
akizungumza na watumishi na baadhi ya viongozi (hawapo pichani)waliohudhuria
hafla ya makabidhiano ya ofsini na Mkuu wa Mkoa mpya Amosi Makala Machi 17
mwaka huu.
|
MKUU wa
mkoa wa Mbeya, Amos Makala, amekabidhiwa rasmi ofisi yake leo na aliyekuwa Mkuu
wa mkoa huo Abbas Kandoro, huku akitoa maagizo manne mazito kwa watumishi wa
serikali.
Makala
alisema kuwa, wakuu wote wa wilaya na wakuu wa idara katika Halmashauri za
wilaya zilizopo mkoa wa Mbeya, kila siku ya Alhamisi kuanzia saa nne mpaka saa
nane mchana ni marufuku kukaa ofisini bali wanatakiwa kwenda kupokea kero za
wananchi vijijini na kuzishughulikia.
“Mimi
sijaja kutengua torati bali kutimiliza. Kila mmoja wetu atimize wajibu wake na
kuacha vyeo vya uadmin wa magroup kwenye Whats App na face book” alisema
Makala.
Alisema
agizo lingine hataki kusikia masuala ya ugonjwa wa kipindupindu katika
Halmashauri za mkoa wa Mbeya, huku akiagiza kuwa lazima mazingira yawekwe safi.
Kuhusu
watumishi hewa wanaolipwa mishahara alisema jambo hilo halihitaji digrii ili
kuelewa na kulitekeleza ndani ya siku 15 kama lilivyo agizo la Rais Dkt. John
Magufuli, hivyo Wakurugenzi na maafisa utumishi wameagizwa kuwabaini haraka.
“Nimekabidhiwa
taarifa hapa na Mkuu wa mkoa mstaafu kaka yangu Abbas Kandoro, najua kuna taarifa
za upungufu wa madawati katika wilaya zetu, hivyo basi kila Mkurugenzi wa
wilaya akaandike barua kuthibitisha alichopeleka kwenye taarifa yake na wala
msidanganye na kuogopa kueleza ukweli ili wakati wanataka kunishughulikia mimi
barua zenu ziwe ushahidi kuwa mlidanganya” alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Aliwaeleza
kuwa yeye kwa umri wake siyo mtu wa kukaa ofisini na kauli mbiu yake ni kwamba
walipo wananchi, palipo na kero naye yupo na kwa sasa chini ya serikali ya
awamu ya tano wanacheza mchezo uitwao usiniguse.
Kwa upande
wake aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Abbas Kandoro, alisema kuwa anawashukuru
sana marais wote wa Tanzania kwa kufanya kazi nao na sasa anastaafu akiwa na
miaka 66 ambapo ametumikia taifa hili kwa miaka 40.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA, AMOS MAKALA, ATOA MAAGIZO MANNE MAZITO KWA WATUMISHI WA SERIKALI.”
Post a Comment