Wednesday, February 22, 2017

RAY C, AKUMBANA NA MAJANGA MENGINE


Msanii wa bongo fleva Ray C amefukuzwa kwenye lebo ya wanene Enterteiment baada ya kauli ya yake aliyodai  kwamba hajasaini na lebo yeyote.
 Maneja wa Wanene Enteriment Gentriz amesema kuwa Ray C alikuwa kwenye hatua za mwisho kuweza kusajiliwa katika lebo ya Wanene ila alikosea baada ya kupewa demo ya nyimbo yake ambayo ilikuwa haijawa tayari na kuivujisha hali iliyopelekea uongozi wa wanene kukasirika na kuamua kumtimua.
Hata hivyo Ray C alivyoongea kupitia eNewz alisema sababu iliyopelekea yeye kufanya kazi na wanene ni baada ya kupewa ofa ya kurekodi na lebo hiyo ya Wanene hali iliyompelekea kushindwa kukataa kwa kuwa wanene ni lebo kubwa na yenye vyombo vya kisasa zaidi.

0 Responses to “RAY C, AKUMBANA NA MAJANGA MENGINE”

Post a Comment

More to Read