Wednesday, March 1, 2017
MBUNGE MBARONI KWA KUBAKA
Do you like this story?
MBUNGE
wa Imenti ya Kati, Gideon Mwiti anayekabiliwa na shtaka la ubakaji
Jumanne aliomba mahakama ya Milimani nchini kenya iorodheshe kesi hiyo
kusikizwa baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8, 2017 kufanyika.
Mwiti
ambaye amekanusha shtaka hilo alimweleza hakimu mkuu Bw Francis Andayi
kwamba 'anatazamia kutetea kiti hicho cha Imenti ya Kati na angetaka
kesi iahirishwe ili apambane na wapinzani wake'.
Wakili
Dkt John Khaminwa anayemwakilisha Bw Mwiti alimweleza hakimu kwamba,
mahakama ndiyo kilele cha demokrasia na mtetezi wa haki za binadamu kuu
zaidi.
Akasema
Dkt Khaminwa: “ Mheshimiwa, mshukiwa katika kesi hii ni mwanasiasa na
atakuwa anawania kiti cha uwakilishi bungeni. Naomba kesi dhidi yake
itengewe siku baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8, 2017.”
Kiongozi
wa mashtaka Bw Eddie Kadebe alipinga ombi hilo akisema 'kortini
kunashtakiwa wavunjaji wa sheria peke yao na wala sio taaluma wala
nafasi za watu zinazoshtakiwa'.
Kadebe
alimweleza hakimu: “Naomba hii korti itilie maanani kwamba
wanaoshtakiwa mahakamani ni wavunjaji wa sheria na wala sio taaluma za
washukiwa. Iwapo ni daktari au mjuzi au mwanasaikolojia au mpasuaji
maiti au taaluma yoyote. Naomba korti iendelee na kesi dhidi ya Mwiti
kulingana na kalenda ya mahakama.”
Hakimu aliamuru kesi hiyo iendelee Machi 24.
Mwiti ameshtakiwa pamoja na daktari ambaye anadaiwa alikuwa anawapima wanawake kutambua ikiwa walikuwa na Ukimwi au la.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)