Saturday, March 18, 2017
MWAKYEMBE ARINGIA OFISI YAKE
Do you like this story?
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk
Harrison Mwakyembe amesema tangu aingie katika wizara hiyo, wameboresha
mazingira ya kisheria na ya mahakama.
Akizungumzia mjini Morogoro katika ziara
ya siku mbili, pia ametoa wito kwa wananchi kuwaripoti mahakimu
wanaokwenda kinyume kwenye kamati za maadili ambazo zimeundwa kila
wilaya zikiwa chini ya wakuu wa wilaya ambao ni wenyeviti na makatibu
tawala wa wilaya ni makatibu.
“Mkiwaona mahakimu ama kwa vitendo vyao,
mwenendo, matamshi au wanakiuka kutenda haki, muwaripoti katika kamati
hizi ambazo zina nguvu na zimeundwa maalumu kupunguza malalamiko ya
wananchi. Uamuzi wa kamati hizi unakwenda hadi Tume ya Utumishi ya
Mahakama,” amesema.
Akizungumzia biashara ya fedha, amewaonya
wananchi kutojihusisha na kukopesha fedha bila kuwa na kibali cha Benki
Kuu ya Tanzania (BoT), kwa kuwa ni kujihusisha na biashara haramu jambo
ambalo halitavumiliwa.
Awali, Dk Mwakyembe amesema kuanzia mwezi
Mei hakutakuwa na ndoa itakayofungwa nchini bila wahusika kuwa na vyeti
vya kuzaliwa, lengo likiwa ni ili Taifa liweke vizuri kumbukumbu za raia
wake.
Amewataka watu waliotajwa kisheria kuwa
wanaweza kufungisha ndoa, wajiandae kutekeleza agizo hilo na kwamba
uamuzi huo utakuwa ni wa lazima kwa kila mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWAKYEMBE ARINGIA OFISI YAKE”
Post a Comment