Saturday, March 18, 2017
MWANAMITINDO AGONGWA NA TRENI AKIPIGA PICHA
Do you like this story?
Mwanamitindo
Fredzania Thompson aliyekuwa na umri wa miaka 19 amefariki dunia baada
ya kugongwa na treni huko Texas, Marekani wakati akipigwa picha.
Mamlaka zinasema kuwa Thompson alikuwa amesimama katikati ya reli
pale ambapo treni ya BNSF ilipokuwa inakaribia. Alitoka kwenye reli
lakini hakugundua kuwa treni ya umoja wa Pasifiki ilikuwa ikija kutokea
upande mwingine wa reli na akagongwa.
Hakamie Stevenson ambaye ni baba wa binti huyo alieleza kuwa binti
yake alisoma chuo cha Blinn kilichopo Bryan, Texas na alitamani
kujiingiza katika masuala ya mitindo. “Hicho ndicho alichokuwa anakitaka
haswa. Na ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza siku hiyo aliyogongwa na
treni.” Alisema Baba wa Thompson
Aliyekuwa akipiga picha hizo hakuumia. Justin LEETH, mkuu wa polisi
wa Idara ya Polisi Navasota aliiambia CNN kuwa”Kwa sasa bado
hatujagundua kama kuna hila yoyote iliyosababisha kifo chake,”
Mchumba wake alieleza kuwa wiki mbili zilizopita Thompson alimwambia kuwa ni mjamzito.
“Alikuwa akiwasaidia sana ndugu zake, na alihakikisha kuwa kila kitu
kinafanyika kwa tahadhari, alikuwa kiongozi mzuri.” Alisema mama yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWANAMITINDO AGONGWA NA TRENI AKIPIGA PICHA”
Post a Comment