Friday, March 17, 2017

EFC BANK YAANZISHA HUDUMA MPYA YA MTANDAO WA BIASHARA "EFC BUSINESS NETWORK" KWA WATEJA WAKE


Mkurugenzi Mtendaji wa EFC Bank Bw. Bas Nierop akizungumza na wateja katika Uzinduzi huo

 

Benki ya EFC Tanzania Microfinance Bank Ltd leo imezindua huduma mpya kwa wateja wake ya mtandao wa kibiashara wenye lengo la kuboresha mawasiliano kati ya wateja na benki itakayosaidia  kurahisisha utoaji huduma  hasa katika shuguli zao za ukopeshaji, ambapo  Benki hiyo inaamini mawasailiano mazuri na mteja ni jambo muhimu katika kipindi hichi ambapo benki inakua kwa kasi.


Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Makao makuu ya Benki hiyo yaliyopo maeneo ya Victoria Barabara mpya ya Bagamoyo Jijini Dar es slaam  Mkurugenzi mtendaji Bwana Bas Nierop amesema EFC sasa ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha inaongeza matawi yake Dar es salaam na  Mikoani ili kuweza kuwasogezea wananchi huduma za kibenki na mikopo kwa ukaribu zaidi.


Aidha bwana Nierop ameongeza kuwa miaka sita sasa imepita tangu EFC ianze kutoa huduma zake kama taasisi ya mikopo na imekuwa ikijiendesha vizuri kwa kutoa  huduma nzuri kwa wateja wake kiasi kwamba wameiona ipo haja ya kutanua wigo wa kibiashara na kuwa Benki kamili yenye uwezo wa kutoa mikopo  kwa wajasiliamali na kuwahudumia kibenki zaidi, ambapo wataweza kutoa na kuhifadhi fedha kwa usalama zaidi nakunufaika na huduma hiyo.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mikopo Bw. Robert Pascal akisisitiza Jambo kwa wateja


Nae Mkurugenzi wa kitengo cha mikopo Bwana Robert Pascal amesema katika kuboresha huduma zao Benki hiyo imeanzisha utaratibu wa kukutana na wateja wake mara kwa mara  ili kuweza kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wateja wao na kuona namna bora ya kuboresha huduma zao kwa wateja wao.Pia bwana Pascal kawasisitiza wateja kua waaminifu ili kujenga mahusiano mazuri na benki.

Baadhi ya wateja waliohudhuria uzinduzi wa EFC Business Nertwork


Meneja masoko wa Benki hiyo Bi Waheeda Mohamed amewataka wakazi wa Dar es salaam kuchangamkia fursa ya kujiunga na benki yao kwani sasa benki hiyo imeweza kupiga hatua na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo  mikopo  kwa masharti nafuu ambayo hata Mwananchi wa kwaida anaweza kumudu.

 Picha na Khalid Mhina. 

0 Responses to “EFC BANK YAANZISHA HUDUMA MPYA YA MTANDAO WA BIASHARA "EFC BUSINESS NETWORK" KWA WATEJA WAKE”

Post a Comment

More to Read