Friday, March 17, 2017

MADEREVA 16 WA GARI ZA MAFUTA WAZUILIWA KUVUKA FORODHANI TUNDUMA KWA MIEZI MIWILI


Madereva wa gari 16  za masaafa marefu za kampuni ya Z.H. Pope Limited  inayosafirisha mafuta kwenda nchi za nje  wameilalamaikia mamlaka ya mapato TRA  forodha ya Tunduma mkoani Songwe kwa kuwazuia kuvusha magari yao tangu January mwaka huu huku wakitaja kuwa licha ya kukumbana na hasara ya mali inayosafirishwa lakini pia wametahadharisha kuwa aina ya bidhaa inayosafirishwa ni hatari  kukaa muda mrefu eneo la makaazi ya watu.

Madereva hao wamesema kuwa tangu tarehe 19 mwezi January 2017 gari 16 za kampuni ya Z.H Pope Limited ya jijini Dar es Salaam zimezuiliwa na mamlaka ya mapato TRA forodha ya  Tunduma - Nakonde, ikielezwa kuwa bado yanadaiwa,  huku wakitaja kuwa gari hizo zimebeba vimiminika hatarishi kwa maegesho yaliyo katikati ya maeneo yanayozungukwa na shughuli  za kibanadamu.
Nimezungumza na meneja wa mamlaka ya mapato TRA ambaye amesema kuwa magari hayo yamezuiwa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu za forodha baina ya mlipakodi  na  TRA.
Kuhusu hatari ya kuegesha magari  yenye mafuta ambayo ni vilipukizi meneja Chembo amesema kuwa tahadhali iliyopo sio jukumu la TRA pekee bali ni kwa wadau wote ikiwemo zimamoto na halmashauri kuhakikisha usalama katika maeneo ya maegesho.

0 Responses to “MADEREVA 16 WA GARI ZA MAFUTA WAZUILIWA KUVUKA FORODHANI TUNDUMA KWA MIEZI MIWILI”

Post a Comment

More to Read