Friday, March 17, 2017
WAFANYABIASHARA WA VIROBA WALALAMIKIA HASARA
Do you like this story?
Baadhi
ya wauzaji wa vileo kwenye manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa,
wameulalamikia utaratibu wa jeshi la polisi mkoani humo, wa kudhibiti
pombe zilizoko kwenye vifungashio vya plastiki maarufu kama viroba,
kwani hauwatendei haki na kuzidi kuwatia hasara ya kuwa na shehena ya
pombe isiyouzika, na wakipekuliwa mara kwa mara huku wakiwa na mikopo
kwenye mabenki mbalimbali.
Wakiongea mjini Sumbawanga wauzaji hao wa vileo, wamesema askari wa jeshi la polisi wamekuwa wakiwavamia mara kwa mara kufanya upekuzi kama bado wana shehena hiyo ya viroba, bila hata ya kufuata utaratibu hali inayoashiria kuwepo kwa uhitaji wa rushwa, huku hadi sasa wakilizuia lori aina ya scania lililokamatwa na katuni 365 za pombe hizo za viroba likitokea jijini Mbeya, hali inayomfanya mfanyabiashara huyo kulipia gharama ya gari hilo kutofanya kazi kwa mmiliki.
Kwa upande wake kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa kamishna msaidizi wa polisi George Kyando, amesema yupo tayari kukutana na wafanyabiashara hao walio tayari kusalimisha shehena za viroba walizonazo, ili kupanga namna ya kuzihifadhi hadi hapo utaratibu mpya utakapotolewa, kwani wengine walinunua bidhaa hizo kabla ya zuio kutolewa na serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAFANYABIASHARA WA VIROBA WALALAMIKIA HASARA ”
Post a Comment