Friday, April 28, 2017
BAADA YA MANARA, KADI TATU ZA FAKHI ZATUA KWA MJUMBE WA YANGA
Do you like this story?
Bodi ya ligi Tanzania imemfungulia mashitaka, Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji wa klabu ya Yanga, Salum Mkemi, mbele ya Kamati ya Nidhamu ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Taarifa ya Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura imesema
kwamba Mkemi aliishutumu na kuidhalilisha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa
Ligi, ijulikanayo kama Kamati ya Saa 72, kupitia vyombo vya Habari kwa kusema
inaendeshwa kiunazi na imegubikwa na rushwa.
Wambura amesema Mkemi aliishitumu Kamati ya Saa 72, iliamua suala
la kadi tatu za njano za mchezaji Mohammed Fakhi Gharib wa Kagera Sugar kwa
upendeleo kutokana na rushwa waliyopewa na Simba SC.
Aidha, Wambura amesema madai ya Mkemi sio ya kweli na yana lengo
la kuwakashifu na kuwadhalilisha viongozi wa TFF na Kamati ya Saa 72 mbele ya
mashabiki wa mpira miguu na Watanzania kwa ujumla.
“Kutokana na kitendo hicho ambacho kina lengo la kusababisha
vurugu kwenye mpira wa miguu, tunaomba mlalamikiwa aadhibiwe kwa mujibu wa
ibara ya 53 (1) na (2) ya kanuni za Nidhamu za TFF pamoja na kanuni ya 41 (2)
ya Ligi Kuu,”amesema Wambura na kuongeza; “Pia apewe adhabu nyingine kama
ambavyo Kamati ya Nidhamu itaona inafaa kwa kuzingatia Kanuni za Nidhamu za TFF
toleo la 2012,”.
BY HAMZA FUMO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BAADA YA MANARA, KADI TATU ZA FAKHI ZATUA KWA MJUMBE WA YANGA”
Post a Comment