Wednesday, April 19, 2017
Kishindo cha Prof. Kitila chaanza na DAWASCO
Do you like this story?
Katibu mkuu wa wizara ya maji
Prof: Kitila Mkumbo amelitaka shirika la maji safi na taka nchini
DAWASCO kuhakikisha wanawekeza sana kwenye usambazaji wa maji kwani ni
aibu kwa jiji la Dar es salaam kuwa na maeneo ambayo hayana maji.
Prof Kitila Mkumbo (Kushoto)
Prof:
Kitila Mkumbo ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es salaam wakati
alipofanya ziara katika shirika hilo na kukutana na watendaji wakuu wa
DAWASCO pamoja na watendaji wakuu kutoka Mamlaka ya maji safi na taka
jijini Dar es salaam DAWASA.
“Pamoja na kazi nzuri
mnayofanya ya kuhakikisha upatikanaji wa maji hakikisheni mnaongeza kasi
ya usambazaji wa huduma hii muhimu kwa wananchi kwa kufanya hivyo
mtakuwa mnatendea haki dhana ya kuwa mnaongoza kwa mapato lakini pia
mnatoa huduma stahiki kwa wananchi”. Alisema Prof. Kitila
Pamoja na hayo amewasii wateja wote wa
DAWASCO kutii agizo la Mhe. Rais kwa kulipia huduma wanazozipatiwa ili
kuziwesha mamlaka hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Prof: Mkumbo pia amelitaka shirika hilo
kukamilisha miradi ya maji katika maeneo ambayo mpaka sasa inaonekana
haijakamilika kwa lengo la wananchi kupata maji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “Kishindo cha Prof. Kitila chaanza na DAWASCO”
Post a Comment