Wednesday, April 19, 2017
Upendo Nkone amuangukia JPM akiomba ubunge
Do you like this story?
Mwanamuziki wa injili, Upendo
Nkone amesema yuko tayari kutumikia nafasi ya ubunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo Rais Magufuli atamteua.
Akiwa
katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Upendo alisema, anaamini
ametumwa na Mungu kufikisha ujumbe wake kupitia uimbaji, lakini pia yuko
tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge, na kuweka wazi kuwa
si kwa ubunge wa kugombea jimboni.
"Sina mpango wa kuwa
mwanasiasa, kwahiyo hata ubunge wa kugombea siwezi, lakini kama Rais
wangu Magufuli akilala akiota kwamba anipe ubunge viti maalum, kwakweli
napokea.... Mh. Magufuli nimeambiwa nigombee ubunge, basi unikumbuke
baba" Amesema Upendo
Amesema aliwahi kushauriwa kugombea ubunge katika jimbo fulani lakini hakuwa tayari kwa kuwa hapendi kugombea.
Akieleza sababu kuu ya kutopenda ubunge
wa kugombea, amesema masharti ya kugombea ni lazima uwe kwenye vyama vya
siasa jambo ambalo halipendi.
Jambo lingine amesema mchakato wa kupata
ubunge wa kugombea ni mgumu una mambo mengi ikiwa ni pamoja na gharama,
jambo ambalo haliwezi na hivyo kusisitiza kuwa Rais Magufuli anapaswa
kumkumbuka katika nafasi zake za kutea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “Upendo Nkone amuangukia JPM akiomba ubunge”
Post a Comment